Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Pius Maneno imebainisha kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya Pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa Hesabu (ATEC I , ATEC II) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya Awali/Msingi (Foundation Level) yenye masomo matano, Hatua ya Kati (intermiediate Level), yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye masomo manne.
"Watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 6,401 kati ya hao watahiniwa 633 sawa na asilimia 9.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 5,768 sawa na asilimia
90.1. Kati ya watahiniwa hao 2,763 sawa na asilimia 47.9 ni wanawake na 3,005 sawa na asilimia 52.1 ni wanaume.
Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 162 ambao ni asilimia 6.5 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 24 sawa na asilimia 0.7 wamefaulu kwa kufaulu masomo walioyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 708 sawa na asilimia 12.5 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza," alisema Maneno.
Pia alisema watahiniwa 894 sawa na asilimia 15.5 wamefaulu mitihani yao na kwamba watahiniwa wengine 2,624 sawa na asilimia 45.5 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali na watahiniwa 2,250 waliobakia sawa na asilimia 39.0 hawakufaulu mitibani yao.
Awali, taarifa hiyo ilieleza kuwa watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 709 kati ya hao watahiniwa 60 sawa na asilimia 8.5 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo kufanya ndani ya watahiniwa waliofanya mitihani kuwa 649 sawa na asilimia 91.5.
Pia imeelezwa kuwa kati ya watahiniwa 649 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 95 ambao ni asilimia
14.6 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku wengine 02 sawa na asilimia 0.3 wamefaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 112 sawa na asilimia 17.3 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza.
Imeelezwa kwa ujumla watahiniwa 209 sawa na asilimia 32.2 wamefaulu mitihani yao na watahiniwa 312 sawa na asilimia 48.1 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 128 waliobakia sawa na asilimia 19.7 hawakufaulu mitihani yao.
Aidha, katika hatua ya Kati, waliojisaliwa walikuwa 3,275 kati ya hao watahiniwa 379 sawa na asilimia 11.6 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 2,896 sawa na asilimia 88.4. Kati ya watahiniwa 2,896 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 28 ambao ni asilimia
1.0 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 19 sawa na asilimia 0.7 wamefaulu kwa kufaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma.
Alisisitiza kuwa wengine 302 sawa na asilimia 10.4 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza, hivyo Kwa ujumla watahiniwa 349 sawa na asilimia 12.0 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 1,372 sawa na asilimia 47.4 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 1,175 waliobakia sawa na asilimia 40.6 hawakufaulu mitihani yao.
Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 2,159 kati ya hao watahiniwa 181 sawa na asilimia 8.4 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanua mitihani walikuwa 1,978 sawa na asilimia 91.6. Kati ya watahiniwa 1,978 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 21 sawa na asilimia 1.1 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, mwingine 01 sawa na asilimia 0.1 amefaulu kwa kufaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma.
Amesema watahiniwa 268 sawa na asilimia 13.5 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 832 sawa na asilimia 42.0 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 856 waliobakia sawa na asilimia 43.3 hawakufaulu mitihani yao.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...