Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHULE ya Ukunga na Uguuzi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan(AKU) imetumia maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU)kufafanua kwa kina kuhusu programu zake mbalimbali ambazo zinatolewa chuoni hapo na kuwataka wanafunzi kuomba kujiunga na chuo hicho.

Akizungumza leo Julai 27,2021 wakati maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Mhadhiri wa Shule ya Ukunga na Uuguzi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU) Profesa Tumbwene Mwansisya amesema wapo kwenye maonesho hayo kwa lengo la kuzungumza na watanzania kuhusu chuo hicho.

"Sisi Shule ya Ukunga na Uuguzi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan tuko kwenye maonesho ya TCU na tumeleta programu mbalimbali ambazo wanafunzi wanaweza kuomba.Kwanza tueleze tuna vitivo vitatu ambavyo ni Udaktari , Uuguzi na Ualimu.

"Tukianza na Uuguzi tunatoa shahada ya uuguzi, tunatoa shahada ya uuguzi kwa wale ambao wameshakuwa wauguzi ambao wanakuwa na kiwango cha diploma wanakuja kufanya Digrii.Pia tnatoa Shahada ya Uzamili ya Ualimu, kwa hiyo tunatoa kwa njia mbili ya full time na part time.Full time ni mwaka mmoja na ile part time inaweza kwenda hadi miaka mitatu,"amesema.

Ameongeza kwa upande wa Udaktari wanazo programu tano ambapo wanatoa Shahada za Uzamili na kwamba hawana shahada ya kwanza."Kwa hiyo katika shahada ya uzamili , tunashahada ya uzamili ya magonjwa ya ndani, shahada ya uzamili ya watoto, tuna shahada ya uzamili ya familia medicine na tunayo shahada ya uzamili nyingine ambayo ni mpya ni ya magonjwa ya akina mama.

"Shahada zote za Uzamivu ni zile ambazo zinahusu spesolisti, kwa hiyo tunaprogramu tano katika udaktari na tumekuja kwenye maonesho haya ili kuonesha programu tunazo ambazo nyingi wanafunzi wetu wanajifunza kwa vitendo,"amesema.

Amesisitiza kutokana na elimu ambayo wanaitoa chuoni kwao, wanafunzi wanaopita kwenye mikono yao wanakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi kokote wanakokwenda.

Katika maonesho hayo , Serikali kupitia Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zena Mohamed Said ametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina mikakati inayoendelea kufanywa na Serikali katika kuweka mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu.

"Awamu ya sita itaendeleza kazi nzuri ya miaka mitano iliyopita, aidha tutajielekeza kufanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 na kufanya marekebisho kwenye mitalaa iliyopo ili ielekezwe kwenye kutoa elimu na ujuzi kulingana na mazingira ya nchi na soko la ajira.

"Hivyo tunatarajia katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya sita kutakuwa na mapitio ya kuiboresha sekta ya elimu ili iendane na mazingira ya sasa ili kukidhi mahitaji ya kijamii, kichumi na soko la ajira pamoja na kuwasomesha na kuwandeleza wanatalaama na watalaamu nchini.

"Ili kuwa na idadi ya wanataaluma wanaoendana na ongezeko la udahili wa vyuoni na wenye taaluma ya viwango vya kitaifa na kimataifa.Serikali tunatambua mchango wa wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi ambao wamejielekeza katika utoaji wa elimu kwa ngazi zote kuanzia elimu,"amesema,
Amefafanua kutokana na takwimu zilizopo ni wazi mchango wa sekta binafsi ni mkubwa katika kuendeleza na kutoa huduma ya elimu nchini,hivyo serikali inatambua na kuthamini mchago wao wa kutoa elimu bora bila kujali itikadi za kisiasa wala imani za kidini.


"Serikal itaendelea kushirikiana nanyi kwa karibu na kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili kuhakikisha azma ya Serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi wote inafanikiwa.Natoa mwito kwa washiriki wote wa maonesho haya kujitathimini ni kwa namna gani taasisi zetu zimekuwa sehemu ya ufumbuzi wa changamoto zetu na kuwa chachu ya maendeleo ya taifa letu."Amesema.
 Mratibu Masoko na Mawasiliano wa Shule ya Ukunga na Uuguzi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU), Maria Chilipachi Kisanko, akiwapa maelekezo wanafunzi namna ya chuo hicho kinavyotoa huduma zake kwa Watanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar Zena Said akitembelea banda ya Chuo Kikuu cha Moshi wakati alipotembelea maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania( TCU).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...