Na Farida Saidy Morogoro.


Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA inaraani kitendo Cha Wananchi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora cha kukata Mkia na Mkonga wa Tembo aliyeingia kwenye kisima wakati akijitafutia chakula katika Msitu wa Unyambui uliomo katika Wilayani humo.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo ilisema kuwa mnamo tarehe 22.07.2021majira ya saa 8 mchana mamlaka ilipokea taarifa toka kwa Afisa Wanyamapori Wilaya ya Igunga kuwa katika msitu wa Unyambiu Kuna tembo alidumbukia kwenye kisima kilichopo Kijiji Cha Kityelo na kutolewa baadhi ya viongo vyake.

Aidha taarifa hiyo ilisema kuwa Tembo huyo alikutwa akiwa mahututi, huku watu wasiojulikana wakiwa wamemkata mkia na mkonga suala ambalo lililosababisha kifo chake na kuliingizia Taifa hasala.Msitu wa Unyambiu umekuwa ulitumiwa na tembo kwa nyakati tofauti huku Uvamizi wa shughuli za kibinadamu Katika msitu huo huwafanya tembo kutoka mara kwa mara na kuingia Katika Vijiji ambavyo vipo jirani na msitu huo.

Hata hivyo Mamlaka anatoa wito kwa waananchi kutoa Taarifa kwa wataalamu wa wanyamapori ili hatua stahiki zichukuliwe wanapoona wanyamapori wakali kwenye maeneo yao pamoja na matukio ya tembo kuvamia kwenye mashamba.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...