Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata amewataka wadau wa mapato jiji la Arusha kuzingatia matumizi ya mashine ya kielektoniki EFD kwa usahihi kulingana na kampeni iliyoanzishwa ya matumizi ya mashine hizo.
Akizungumza katika mkutano na wadau hao,Kidata amewataka pia kuzingatia kwa ukamilifu utunzaji wa kumbukumbu za biashara ili kuweza kuisaidia mamlaka na wafanyabiashara kuenenda kwa pamoja na kuweza kukuza uchumi wa nchi kwa ulipaji kodi kwa hiyari.
"Utunzaji wa kumbukumbu ni suala muhimu sana katika ukadiriaji na ukusanyaji wa kodi hivyo ni muhimu wafanyabiashara wote tutunze kumbukumbu ili kuwezesha maofisa kukadiria kodi kwa usahihi."alisisitiza Kamishna Kidata
Aidha amesema siyo matarajio ya serikali kukusanya kodi zisizo za msingi hivyo kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mashine za EFD kufuatia taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mwaka 2020 iliyomtaka kila mfanyabiashara kununua na kutumia mashine hizo zenye uwezo wa kuandika majina na namba ya utambulisho ya mnunuzi wa bidhaa au huduma kwa faida ya mnunuzi na muuzaji.
Vilevile ameongeza kuwa TRA imeboresha mfumo wa EFD wenye uwezo wa kuunganishwa na mfumo wa uhasibu wa mlipa kodi bila kumlazimu mteja kununua mashine hiyo na kusema kuwa mamlaka ya mapato Tanzania imeanza kampeni yenye lengo la kuhakikisha kila mfanyabiashara anatumia mashine sahihi na kutoa risiti kwa kila mauzo sahihi.
"Labda niseme tu zoezi hili kwa kweli halitamuacha mtu yeyote awe muuzaji au mteja,na tusingependa kumuona mlipa kodi wetu anapata adhabu zisizo za lazima kwani kudai risiti na kutoa risiti kwa kola manunuzi yanayofanywa ni jambo la msingi sana na kwenye hili tutatumia sheria kutoa adhabu kali ambayo haipungui milioni 3 au kifungo au vyote kwa pamoja."aliongeza Kamishna huyo
Sambamba na hayo amesisitiza ulipaji kodi wa hiyari pamoja na uandaaji wa ritani za kodi kwa usahihi na uwasilishaji wa ritani hizo kwa wakati kwa njia iliyorahisishwa ya mtandao lwa kutumia mfumo E-FILING TAX RETANS sambamba na kuzingatia matumizi ya stape za ushuru ambapo mfumo huo unalenga wazalishaji wa bidhaa zinazotozwa kodi kwa mujibu wa sheria za ushuru wa bidhaa hususani maji,soda,sigara,bia na pombe kali.
"Mfumo huo unafaida nyingi ikiwemo udhibiti na kuongeza usalama katika usambazaji na masoko kwani biashara hizi zimekuwa na changamoto ya kugushiwa ambazo huatarisha afya na usalana wa walaji."
Ameeleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuona uchumi unakuwa kwa kuweka mazingira salama,rafiki,wezeshi na yenye usawa kwenye biashara ambapo mfumo wa ETS unaongeza uwazi na ufanisi katika ukusanyaji wa ushuru wa stape.
Kamishna Kidata amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya arejesho ys forodha kwenye sukari na amesema kawaida ushuru huo ni asilimia 10,ili kulinda upotevu wa mapato ya serikali wenye viwanda walitakiwa kuweka dhamana ya asilimia 15 ambayo baadae hurejeshewa ambapo katika kipindi cha juni 2020 hadi mwezi mwaka huu jumla ya marejesho yaliyokuwa yanadaiwa ni bilioni 57,baada ya uhakiki jumla ya shilingi bilioni 8.7 hazikukidhi vigezo na jimla ya shilingi bilioni 49 zilikidhi vigezo huku bilioni 37.7 zimerejeshwa kwa waliokuwa wanadai.
"Kupitia sheria ya mwaka huu wa fedha takwa la kuweka dhamana ya asilimia 15 imeondolewa hivyo kuondoa kilio cha wafanyabiashara kushikiliwa mtaji wenu."alisema
Naye mmoja wa wadau hao Willbroad Chamburo ameomba wafanyabiashara kupewa elimu juu ya sheri za kodi kwani sheria zilizopo haziendani na mfumo wa kazi Tanzania
"Kodi yote ya serikali ileteni kwa hiyari na tusingependa kama mamlaka kurudi wakati wa nyuma kwenye matumizi ya nguvu katika ukusanyaji wa kodi,tengenezeni mipango ya ulipaji wa madeni ya nyuma na lipeni hata ukishindwa kulipa deni lote kwa wakati mmoja basi omba ulipe kidogo kidogo ili ulimalize ndani ya muda utakao pangiwa."Alisema
Awali akizungumza katika mkutano huo Kaimu Kamishna wa walipakodi wakubwa Bwn.Beatus Nchota amesema kuwa mkutano huo umefuatia baada ya kikao walichokaa na wadau hao cha kusikoliza changamoto ya mteja mmoja mmoja.
Home
BIASHARA
TRA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUZINGATIA MATUMIZI YA MASHINE YA 'EFD' KWENYE HUDUMA ZAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...