Meneja wa kampuni ya Safari Automotive Rosalia Mosha (Kulia,) akizungumza na waandshi wa habari baada ya kumkabidhi gari walilolibadilisha muonekano kwa msanii wa nyimbo za asili na sanaa ya jukwaani Mrisho Mpoto na kumwelezea msanii huyo kuwa ni mzalendo na mwenye kuleta hamasa katika jamii leo Mkoani Dar es Salaam.



Msanii wa nyimbo za asili na mtunzi Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba (kulia,) akiwa katika picha ya pamoja  na Meneja wa Safari Automative Rosalia Mosha (kushoto,) mara baada ya kumkabidhi gari lililofanyiwa marekebisho na kampuni hiyo. 




Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba akishangilia pamoja  kikundi chake cha sanaa kilichomsndikiza kuchukuwa gari lake lililobadilishwa muonekano na kampuni ya Safari Automotive leo Mkoani Dar es Salaam.


Msanii wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba (katikati,) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Safari Automotive mara baada ya kukabidhiwa gari lake aina ya Prado leo Mkoani Dar es Salaam.


MSANII Wa muziki wa asili na sanaa ya jukwaani Mrisho Mpoto maarufu kama 'Mjomba' leo Julai 12 amekabidhiwa gari lake liliofanyiwa matengenezo na kubadilishwa muonekano na kampuni ya Safari Automotive bure kabisa ikiwa sehemu ya kutambua mchango wake katika jamii hasa kupitia kampeni mbalimbali anazozifanya katika kujenga jamii imara ikiwemo kampeni ya 'Nyumba ni Choo.'

Akizungumza leo Mkoani Dar es Salaam wakati akipokea gari lake lililobadilishwa muonekano na kampuni ya Safari Automotive Mpoto amesema, Baada ya kuzunguka na gari hiyo katika mikoa mbalimbali nchini katika kampeni ya Nyumba ni Choo muonekano wa gari hiyo uliharibika na kupelekea kufanya maamuzi ya kutaka kuuliuza kabla ya Safari Automotive kufanya hisani hiyo ya kubadilisha muonekano wa gari hiyo bila malipo yoyote ya ziada.

"Ukiwekeza kwenye mioyo ya watu ipo siku utavuna, gharama za matengenezo kwa gari hii inafikia shilingi milioni 20 ambayo Safari Automotive wamefanya hisani kwa kugharamia kiasi chote cha fedha nina imani wameniona kupitia kampeni mbalimbali za kuhamasisha jamii ikiwemo kampeni ya Nyumba ni Choo iliyoanza mwaka 2016 na kuzinduliwa Desemba 17, 2017 na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa makamu wa Rais kwa kipindi hicho.........Na katika kampeni hii  asilimia 6.5 ya kaya hazikuwa na choo na hadi sasa ni asilimia 1.5 pekee ndio zilizobaki.'' amesema.

Aidha amesema, muonekano waliompa Safari Automotive umempa nguvu zaidi  ya kuendelea kutembelea sehemu nyingi zaidi na kuendeelea kuhamasisha na kujenga jamii imara kwa kushirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Safari Automotive Rosalia Mosha amesema, Mrisho Mpoto ni kioo cha jamii na anaangaliwa na wengi kwa namna nyingi na amekuwa akiwekeza kwa jamii kwa namna mbalimbali na anastahili kupata vitu vzuri kutokana na hamasa anayotoa kwa jamii.

Rosalia amesema, muonekano mpya wa gari ya Mpoto umegharimu shilingi milioni 20 na limebadilishwa muonekano wote ikiwemo rangi, siti, zulia pamoja na kunyosha gari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...