Mwalimu Chuo Cha VETA, Mara Elly Nkonya akionesha Teknolojia ya kifaa Cha kunyunyuzia Dawa ya kuua magugu sambani katika maonesho ya 45 ya biashara kimataifa yanayofanyika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Ekari moja kutumia mizunguko Saba na tofauti na ile ya kubeba mgongoni

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) wabuni kifaa vya cha kunyunyuzia dawa za magugu shambani pamoja na kuua wadudu waharibifu wa mazao shambani.

Kifaa hicho zamani kilikuwa kikitumika kwa kubeba mgongoni kwa sasa unasukuma Kama troli amba kwa hekari moja unazunguka Mara Saba

Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Mwalimu Chuo Cha VETA Mkoa wa Mara Elly Nkonya amesema mashine hiyo imeongezewa uwezo ukilinganisha na ile ya kubeba mgongoni.

Amesema kuwa uwezo wake ni mara 16 tufauti na kutokana na kuweka matundu 16 ambapo mkulima inamrahisishia kuweka dawa katika shamba kwa urahisi.

Amesema wanabuni hivyo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za Kilimo kwani badala kuweka watu sita kwa ekari moja kwa kubebesha watu kumwaga dawa mtu mmoja anaweza kufanya kazi hiyo.

"VETA Kazi yetu ni kutatua changamoto kwa wananchi katika Sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na kuweza kupata matokeo chanya kwa kutoa Suluhu zana."Amesema Nkonya

Amesema mashine hiyo katika mashindano ya ubunifu yaliyofanyika hivi karibuni yamechukua nafasi ya pili hivyo inaonyesha kuwa suluhisho kwa wakulima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...