Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amewataka wazalishaji wa mazao ya viungo chini kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakidhi viwango ili waweze kupata soko la ndani na nje jambo ambalo litawasaidia kuongeza thamani ya bidhaa hizo.
Kigahe ametoa kauli huyo Jijini Dar es salaam wakati uzinduzi wa uzinduzi wa nembo ya viungo Tanzania katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere ambapo amesema maendeleo ayawezi kufikiwa ikiwa hakuna bidhaa bora hivyo ni muhimu wazalishaji kuzingatia viwango vya ubora vinavyotakakiwa.
Amesema nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi inayozalisha kwa wingi bidhaa za viungo na kusisitiza kuwa uwepo wa nembo ya alama ya viungo Tanzania utasaidia bidhaa hizo kutambulika ndani na nje ya nchi.
"Uwepo wa nembo katika bidhaa za viungo utasaidia kwa kiasi kikubwa bidhaa kutambulika ndani ya nchi na nje pamoja na kuweka imani kwa wanunuzi wa bidhaa za viungo"amesema
Kigahe amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvunwa ambapo Serikali inatarajia kuongeza Viwanda vya kuchakata mazao ya viungo kama vile tangawizi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha kimataifa cha biashara ( MARKUP) Safari Fungo amesema uwepo wa nembo katika bidhaa za viungo utasaidia kuitangaza nchi katika bidhaa zinazotoka nchini na kuziongezea thamani.
Amesema sasa wakati umefika kwa wa kutagaza bidhaa zinazozalishwa hivyo ni muhimu wazalishaji kutambua umuhimu wa nembo viungo Tanzania katika bidhaa zao.
Naye Balozi mteule ambaye pia ni Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara (Tantrade) Edwin Rutageruka amesema nembo ya viungo ya Tanzania itasaidia kuitagaza nchi pamoja na kuwasaidia Wafanyabiashara kutambulika kuaminiwa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...