Askofu wa Makanisa ya International Evengelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT), David Mabushi akizungumza katika Kanisa la IEAGT la Mjini Shinyanga

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Askofu wa Makanisa ya International Evengelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) David Mabushi, amewataka vijana wa Kanisa hilo kumtumikia Mungu kipindi cha ujana wao, ili wapate baraka katika maisha yao.
Askofu Mabushi amebainisha hayo leo Jumapili Agosti 22,2021 kwenye hitimisho la wiki ya vijana kanisa la IEAGT ambao wameendesha ibada yote.

Amesema kipindi cha kumtumikia Mungu ni cha ujana na hivyo kuwataka vijana wa Kanisa hilo, wamtumikie Mwenyezi Mungu pamoja na kutangaza kazi yake na kuokoa watu ili waijue kweli.

"Ukitaka kuwa na maisha ya ushindi, lazima ujipange katika siku zako za ujana ndipo kwenye maono, ukishakuwa mzee utabaki kuwa na simulizi tu," amesema mchungaji Mabushi.

Naye, Mwenyekiti wa Idara ya Vijana wa Kanisa la IEAGT Peres Mbogoma, amesema kwa juma zima wamefanya vitu mbalimbali, ikiwamo kutembelea kiwanda cha Jambo  pamoja na kutoa msaada wa chakula kwa watoto wenye uhitaji, ambao wanalelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga.

Aidha, akitoa Mahubiri Janet Yohana, amewataka waumini wa Kanisa hilo, wajitoe kwa bwana, na kutoa muda wao na mali, pamoja na kumtolea Zaka na Sadaka zilizo nona, ili wabarikiwe katika maisha yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi waIdara hiyo ya vijana Kanisani hapo Alfred Benjamini, akisoma taarifa amesema wapo 83, na wamekuwa wakifanya vitu mbalimbali, ikiwamo kuinuana karama na kufanya kazi ya Mungu.

Askofu wa Makanisa ya International Evengelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT), David Mabushi  akiwa na mke wake kwenye hitimisho la wiki ya vijana kanisa la IEAGT Mjini Shinyanga.

Mhubiri Janet Yohana, akitoa neno la Mungu kwenye Ibada Kanisa la IEAGT Mjini Shinyanga

Mhubiri Janet Yohana, akitoa neno la Mungu kwenye Ibada Kanisa la IEAGT Mjini ShinyangaMwenyekiti wa idara ya vijana wa Kanisa la IEAGT Mjini Shinyanga Peres Mbogoma, akitoa neno. Mwenyekiti msaidizi idara ya vijana Kanisa la IEAGT Mjini Shinyanga Alfred Benjamini, akisoma taarifa ya vijana.  Vijana wakiwa kwenye Ibada. Waumini wakiwa kwenye Ibada, ambayo inaongozwa na vijana. Waumini wakiwa kwenye Ibada, ambayo inaongozwa na vijana. Waumini wakiwa kwenye Ibada, ambayo inaongozwa na vijana. Waumini wakiwa kwenye Ibada, ambayo inaongozwa na vijana. Waumini wakiwa kwenye Ibada, ambayo inaongozwa na vijana. Waumini wakiwa kwenye Ibada, ambayo inaongozwa na vijana.
Kwaya ya Vijana wakiimba Nyimbo kwenye Ibada.

Na Marco Maduhu-Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...