Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma za mpya ijulikanayo ‘Bima ya Afya na Maisha’ ikilenga kuwezesha ushirikishwaji wa jamii katika kupata huduma za bima jamii  kupitia familia na vikundi mbalimbali vya kijamii ikiwemo vya vicoba, saccos, wafanyakazi, vikundi  vya whatsApp na vyama vya ushirika .

Huduma hiyo inayopewa amana na Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania inahusisha Bima ya ‘Afya  Salama’ mahususi kwa ajili ya wana familia pamoja na Bima ya ‘Nia Njema’  ambayo ni mahususi kwa ajili ya wana vikundi mbalimbali vya kijamii pamoja na familia zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo, Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka alisema huduma hizo  zinalenga kusaidia nia ya serikali katika kuhakikisha kwamba huduma ya bima ya afya inamfikia kila mtanzania.

“Kupitia huduma ya Bima ya Nia Njema  tunalenga kuwalinda watanzania katika vikundi vyao vya kijamii na kiuchumi na wakati huo huo kuwezesha  ushirikishwaji wa jamii katika mifumo fedha kwa kupitia  bima za jamii ikiwemo vikundi vya vicoba, saccos, wafanyakazi , vikundi vya wafanyakazi, Wajasiriamali, taasisi, vyama vya ushirika, makundi ya WhatsApp, na vikundi vingine vya namna hiyo,’’ alitaja.

Alifafanua kuwa bima ya vikundi inahusisha idadi ya wanachama kuanzia watano na kuendelea ambao wanaweza kuwa wanandugu, wanamtaa au muunganiko wowote huku akibainisha kuwa gharama ya kujiunga kwa mwaka ni Tsh 18,000.

“Utofauti wa bima hii ni kutoa huduma ya bima ya maisha kwa wanakikundi pamoja na familia zao, kwa gharama nafuu, uharaka na kwa utalaamu wa bima za jamii.’’

“Huduma hizi zinapatikana katika mikoa yote nchini na mafao ya bima hutolewa ndani ya masaa 24 hadi 48 baada ya kuwasilisha taarifa na viambatanisho sahihi kutoka kwa uongozi wa kikundi na kujaza fomu ya madai. Utaratibu wa kujisajili ni kupitia kikundi,’’ aliongezea.

Alitaja faida ya za bima hiyo ya kikundi kuwa ni pamoja na kuboresha mafao ya kikundi kwa mahitaji ya wanakikundi, kupunguza usumbufu wa kuchangishana miongoni mwa wanakikundi, kupatikana kwa fedha ndani ya muda mfupi na kupunguza michango ya mara kwa mara kwa wanakikundi

Kuhusu Bima ya Afya Salama Bw Nkaka alisema inalenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa wana familia na inatumika katika hospitali  zaidi ya 372 kote nchini ikiwemo hospitali za serikali na hospitali binafsi.

“Huduma hii inawalenga watu wote wenye umri chini ya miaka 64. Kwa upande wa familia inahusisha watu sita akiwemo mteja anayechukua bima  pamoja na mke au mume wake na watoto wao wanne walio chini ya miaka 18,’’ alifafanua.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Sanlam Bi Klispinana Shirima aliwahakikishia wateja wa huduma hizo kuwa ni bora na zinalenga kuwagusa wana jamii moja kwa moja huku akibainisha kuwa kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa kukidhi matakwa na malengo ya kuanzishwa kwake.

Wakizungumza kwenye hafla hiyo Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios ambae ni mdau mashuhuri wa habari nchini pamoja na mtaalamu wa afya na mdau wa habari nchini Dk Isaac Maro walisema ushiriki wao katika kuzinadi huduma hizo unatokana na umuhimu na uhitaji wake kwenye mazingira ya kijamii kwa sasa.

“Kupitia teknolojia hii mawasiliano kwasasa tuna vikundi vingi vya kijamii kupitia simu zetu na hivyo tumejikuta tupo karibu zaidi katika kusaidia kwenye mambo mbalimbali ya kijamii kupitia michango mbalimbali. Ujio wa huduma kama hii ya bima ya Nia Njema ni suluhisho sahihi,’’ alisema Bi Marios ambae ni balozi wa huduma ya Bima ya Nia Njema.

“Kwasisi ambao tunatumia muda mwingi katika kutoa huduma za kiafya kwa jamii ndio tunaweza kufahamu zaidi umuhimu wa Bima ya afya kwasababu tunashuhudia kwa macho yetu faida za kuwa na bima ya afya na athari  za kutokuwa na bima ya afya. Huduma kama hii ya ‘Afya Salama ni mkombozi kwa wana jamii kiafya na kiuchumi,’’ aliongeza Dr Maro ambae ni balozi wa huduma na Bima Afya Salama.

Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka (Katikati) na Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania Bi Klispinana Shirima (Kulia) wakizindua rasmi huduma mpya ijulikanayo ‘Bima ya Afya na Maisha’ inayowalenga wana familia na vikundi mbalimbali vya kijamii ikiwemo vya vicoba, saccos, wafanyakazi, vikundi  vya whatsApp na vyama vya ushirika. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Mawasiliano wa NBC Bw David Raymond (Kulia) na Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (wa pili kushoto) na Dk Isaac Maro (wa pili kulia)


Kwa mujibu wa Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (kushoto) ambae ni mdau mashuhuri wa habari nchini pamoja na mtaalamu wa afya na mdau wa habari nchini Dk Isaac Maro, ushiriki wao katika kuzinadi huduma hizo unatokana na umuhimu na uhitaji wake kwenye mazingira ya kijamii kwa sasa.

Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania Bi Klispinana Shirima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu huduma  hiyo.

Mmoja wa mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (katikati) akizungumza kuhusu huduma ya Bima ya ‘Nia Njema’ inayowalenga wana vikundi vya kijamii na kiuchumi vikiwemo vikundi vya vicoba, saccos, wafanyakazi , vikundi vya wafanyakazi, Wajasiriamali, taasisi, vyama vya ushirika, makundi ya WhatsApp, na vikundi vingine vya namna hiyo wakati wa hafla hiyo.

Mmoja wa mabalozi wa huduma hizo, Bw Isaac Maro (katikati) akizungumza kuhusu huduma ya Bima ya ‘Afya Salama’ inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa wana familia huku ikitumika katika hospitali  zaidi ya 372 kote nchini ikiwemo hospitali za serikali na hospitali binafsi wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu huduma  mpya ijulikanayo ‘Bima ya Afya na Maisha’ inayowalenga wana familia na vikundi mbalimbali vya kijamii ikiwemo vya vicoba, saccos, wafanyakazi, vikundi  vya whatsApp na vyama vya ushirika. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania Bi Klispinana Shirima (wa pili Kulia), Mkuu wa Mawasiliano wa NBC Bw David Raymond (wa pili kushoto) na Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (kulia) na Dk Isaac Maro (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...