Na Said Mwishehe,Michuzi TV

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetangaza kulisimamisha kwa siku saba Gazeti la Uhuru baada ya kuandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho"Sina wazo kuwania urais 2025-Samia" huku kikimuomba radhi Rais Samia.

Pia chama hicho kimesema Bodi ya Wakurugenzi wa gazeti hilo imechukua auamuzi wa kuwasimamisha kazi watumishi wa watatu pamoja na kuunda Tume ya kuchunguza habari hiyo ya upotoshaji.

Akizungumza leo jiijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo amesema huo ni upotoshaji mkubwa wa kumlisha maneno Rais huyo, hivyo kwa nafasi yake ameamua kulifungia gazeti hilo kwa kutochapishwa kwa muda wa siku saba kuanzia kesho.

Aidha amesema mbali ya kulisimamamisha gazeti hilo kwa siku saba , pia amesema baada ya kutolewa kwa habari hiyo bodi ya wakurugenzi imekutana na kutoa maamuzi ya kuwasimamisha Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Publisher Faustine Sungura, Mhariri Mkuu Ramadhan Athuman Mbwaduke pamoja msimamizi wa zamu aliyesimamia gazeti hilo Rashid Zahoro.

"Naomba kuchukua nafasi hii kumuomba radhi Mwenyekiti wa Chama chetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kulishwa maneno ambayo hakuyasema wakati akihojiwa na BBC, ...Uhuru ni gazeti letu hatuwezi kulikana maana hakuna anayeweza kumkana mtoto wake, hivyo tunamuomba radhi Rais wetu.

"Kuomba radhi peke haitoshi,hivyo kwanza naipongeza bodi ambayo leo baada ya kutoka kwa habari hii ya upotoshaji ilikutana na kutoa maazimio kadhaa, tunawapongeza kwa hatua ambazo zimechukuliwa kwa kuwasimisha kazi waliohusika na uandaaji wa habari hii,"amesema.

Gazeti hilo ambalo limetoka leo Agosti 11,2021 limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia na  Shirika la Utangazaji Uingereza( BBC) yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam .Katika habari yake kuu gazeti hilo limeandika " Sina wazo kuwania urais 2025- Samia".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...