CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam washirikiana na serikali ya Italia katika kukuza vijana wenye weledi katika biashara na Ujasiriamali hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 31,2021 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Nchini Itali hapa nchini, Marco Lombardi amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe wanampango mkakati kwa lengo la kupanua huduma hasa ushirikiano na vyuo vikuu vya ndani ya nchi, vyuo vya ukanda wa Afrika Masharikia, Afrika na nje ya bara la Afrika, na kwasasa wapo katika mazungumzo na Chuo cha Milan kilichopo Itali ili kuweza kuendesha program za pamoja.
Prof. Kusiluka amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinaprogramu moja ambayo ni ya Umahili yaani Masters in Business Admnistration impact in Interprenuership ambayo itaonesha matokeo yanayoonekana.
"Nasisi tunatamani vijana wetu wanaohitimu katika vyuo vikuu hapa nchini wawe wanauwezo wa kuazisha biashara, kuwa na miradi ya kijasiriamali ambayo itakuwa inatoa bidhaa zenye Ubora.
Hata hivyo katika Mazungumzo na balozi wa Italia hapa nchini, Marco Lombard Prof. Kusiluka amesema kuwa wamezungumzia mashirikiano ya pamoja na vyuo vya nchini Itali ili kuwa na ushirikiano kati ya wanafunzi wa nchini Itali na wanafunzi wa nchini Tanzania.
Amesema kupitia balozi wa Italia hapa nchini imani yao ni kuunganisha vyuo vingine vya nchini Itali tofauti na chuo cha Milan ili kuweza kufanya mambo mengi kwa pamoja.
"Ushirikiano huo utakuwa katika kuandika miradi ya utafiti na maendeleo ya jamii pamoja na vyuo hivyo na kuitekeleza nchini Tanzania na nchi nyingine.
"Nasisi tumeona fursa ya kushirikiana na Itali kupitia watalii wengi wanaokuja kutalii hapa nchini hasa Zanzibar kwa kuandaa matamasha kati ya Tanzania na Itali ili Tanzania ijulikane kwa utalii pamoja na eneo la taaluma na elimu ambayo tumebobea." Amesema Prof Kusiluka
Amesema kuwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wako vizuri na wanauwezo wa kufanya kazi vizuri kwahiyo amewatoa wasiwasi wahitimu hapa nchini kwani hata wakienda kwenye mashindano na vyuo vingine wanashindana na kuibuka videdea.
Kwa Upande wake Balozi wa Itali nchini Tanzania, Marco Lombardi amesema lengo la ubalozi wa Itali ni kushirikiana na Tanzania kwani Tanzania imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu sana bado imeona Tanzania inafursa kubwa ya kuandaa vijana katika ujasiliamali ambao wanaweza kufanya biashara vizuri na wafanyabiashara waliopo nchini Itali.
Amesema kuwa Katika taasisi za elimu ya juu hapa nchini wanaweza kutoa elimu na kuwapa ujasili wa kufanya biashara na wadau wa kimataifa waliopo nchini Itali.
Amesema suala la kuongeza tija katika wahitimu wa Vyuo vikuu hapa nchini ni la Kiserikali kwani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya kazi kubwa sana katika kutoa elimu ya ujasiliamali kwa kila kada inayofundishwa hapa nchini.
Prof. Kusiluka amesema kuwa kila chuo kwa sasa hivi vinaboresha elimu kwa kufundisha ubunifu, ujasiriamali ili vijana wanaotoka wawe na mtizamo chanya hasa kwakuweza kujiajiri wenyewe na wawe na ujasili wa kuamini kwamba wao wanaweza kuwa wafanyabiashara wakubwa.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akikabidhiwa kitabu na Balozi wa Itali nchini Tanzania, Marco Lombardi leo alipotembelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Itali nchini Tanzania, Marco Lombardi leo Agosti 31,2021 alipotembelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka akizungumza wakati Balozi wa Itali hapa nchini alipotembelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam leo Agosti 31,2021.
Balozi wa Itali nchini Tanzania, Marco Lombardi akizungumza na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam alipotembelea leo Agosti 31,2021 kwaajili ya kushirikiana katika kutoa elimu ya ujasiriamali na kushirikiana katika biashara kati ya Tanzania na Itali.
Balozi wa Itali nchini Tanzania, Marco Lombardi akionesha kitabu wakati akizungumza na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam alipotembelea leo Agosti 31,2021 kwaajili ya kushirikiana katika kutoa elimu ya ujasiriamali na kushirikiana katika biashara kati ya Tanzania na Itali.
Daktari Coletha Komba akitoa shukurani kwa Balozi wa Italia hapa nchini alipotembelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza leo Agosti, 31, 2021 wakati Balozi wa Itali hapa nchini alipotembelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.


Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam wakisikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka wakati walipotembelewa na Balozi wa Itali hapa nchini.
Balozi wa Itali nchini Tanzania, Marco Lombardi katikati, kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi waliopo mbele wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam leo Agosti 31, 2021 mara baada ya kutembelewa na Balozi wa Itali hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...