Na John Walter-Babati
Maafisa utamaduni Halmashauri ya wilaya ya Babati na Babati Mji, wametakiwa kuwa karibu na wasanii ili kukuza sanaa katika wilaya hiyo.

Wito huo umetolewa na Katibu tawala wilaya ya Babati Halfan Matipula wakati akizungumza na kikundi cha Sanaa ya uigizaji Magugu House of Talent katika Hotel ya White Rose Mjini Babati.

Aidha Matipula amewataka Wasanii kufanya Kazi kwa bidii bila kukata tamaa ili kupata mafanikio katika Kazi zao za sanaa.

"Kazi ya sanaa inalipa cha muhimu ni kujituma bila kuchoka,tujifunze kwa waliofanikiwa hawakukata tamaa." Alisema Matipula

Ikumbukwe kuwa Kikundi cha Sanaa cha Magugu House of Talent (MHT) agosti 8 2021 walipanga kuzindua filamu yao iendayo kwa jina la "Mama mdogo" lakini imeahirishwa.

Uongozi wa MHT umesema wameamua kuahirisha kwa sababu ambazo zimeshindwa kuzuilika hivyo watapanga tarehe nyingine kwa ajili ya uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...