Na Humphrey Shao, Michuzi Tv.

MKUU wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amewashukia watendaji na kutoa maelekezo juu ya usimamizi wa miradi katika Wilaya hiyo.

Jokate ametoa maelekezo hayo ikiwa zimepita siku chache tangu kupita Mwenge wa uhuru na kubaini kuwa miradi mingi inayotekelezwa katika Wilaya hiyo haishirikishi wananchi ipasavyo.

"Nimetoa maelekezo kwa uongozi mzima  wenyeviti wa mitaa, watendaji wa mitaa na wananchi miradi ya maendeleo wnayotekelezwa kwenye maeneo yao. Wananchi wana haki ya kupewa taarifa, viongozi wote wa ngazi hizi za msingi wana haki ya kupatiwa taarifa lakini pia wana wajibu wa kusimamia miradi yote ya maendeleo, kusikiliza wananchi na kutatua kero zao. Lazima viongozi wa ngazi zote wawajibike. "Amesema DC Jokate.

"Tunahitaji Temeke yenye ushirikishwaji, wananchi wasikilizwe, ili pia wananchi nao washiriki kikamilifu kwenye miradi ya maendeleo, hiyo ndio maana halisi ya dhana ya mamalaka ya Serikali za mitaa" Alisisitiza DC Jokate.

DC Mwegelo aliendelea kusisitiza kuwa sasa ni muda wa kujenga Temeke mpya na kamwe hatokubali mtu yeyote kujinufahisha na rasilimali za umma kwa maslahi yake binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...