NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.

Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na Watoto Mwanaidi Ally Hamisi amempongeza Diwani wa kata ya msisima na uongozi mzima wa kata ya msisima kwa kuhamasishana na kukubaliana kujenga sekondari ya kata kwa nguvu za wananchi.

Naibu waziri aliwapongeza alipotembelea kukagua ujenzi wa sekondari ya kata ya msisima na kukabidhi mifuko 32 ya smenti kuwatia moyo wananchi katika hatua njema waliyofikia wananchi hao ya kuhitaji sekondari ya kata ili Watoto wa kata hiyo waweze kupata elimu na kuepukana na adha ya Watoto wao kusoma mbali na wengi kushindwa kuendelea na masomo.

Lengo la ziara ya Naibu waziri huyo wilayani Namtumbo lilikuwa ni kufuatilia sera ya uwezeshaji wanawake kiuchumi namna inavosimamiwa katika ngazi za wilaya na kujionea shughuli zinazofanywa na akina mama hao katika kujiinua kiuchumi.

Aidha Naibu waziri aliwaagiza wanawake kutokubali kunyanyaswa kwa kuendeleza mila potovu zilizopo kwenye jamii bali watumie vyombo vya sheria kudai haki zao pale wanapodai haki zao za msingi na kuwataka pia kutumia mahoteli makubwa kuuza bidhaa zao wanazozalisha ili kupata soko la bidhaa wanazozalisha .

Diwani wa kata ya msisima Fransis Kamenya pamoja na kumpongeza Naibu waziri kwa kutembelea kata hiyo na kujionea shughuli zinazofanywa na wananchi hao alimwambia Naibu waziri huyo kuwa kata hiyo haijawahi kutembelewa na kiongozi wa ngazi ya kitaifa kama yeye akamshukuru kwa kuamua kutembelea kata hiyo na kuingiza katika historia kwa mara ya kwanza kutembelewa na kiongozi wa ngazi ya kitaifa alisema Diwani huyo.

Hata hivyo Diwani huyo alimwomba Naibu waziri kuwa wananchi wa kata hiyo wanaomba shule yao ifunguliwe na ianze kutumika kwa kusoma wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2022 ili kuondoa adha ya wanafunzi wengi kutomaliza masomo kutoka katika kata hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Keneth Ningu alimhakikishia Naibu waziri kuwa ofisi yake itahakikisha inashirikiana na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa shule kubaini mapungufu yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili yafanyiwe kazi ili maombi ya wananchi hao yaweze kutekelezwa kadiri ya walivyoomba.

Dkt Ningu aliongeza kuwa serikali haitawaacha peke yenu katika jambo la maendeleo kama hili bali kuanzia sasa serikali ya wilaya itakuwa bega kwa bega kuunga juhudi za wananchi ili lengo la kuifungua sekondari hiyo liweze kutimia alisema Dkt Ningu.

Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Peres Kamugisha alimwomba Naibu waziri mashirika yasiyo kiserikali ambayo yanasaidia jamii kuja mikoani na wilayani badala ya kubaki katika miji mikubwa kama Dodoma,Dar-es-salaam na kuiacha jamii yenye uhitaji wa huduma hizo zikihangaika na kushindwa kusaidiwa ipasavyo huku wilayani.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina jumla ya kata 21 na katika kata hizo ni kata mbili ambazo hazina sekondari ya kata,kata ya Mputa na kata ya Msisima hali inayofanya wanafunzi wengi wanaojiunga na kidato cha kwanza kutoka katika kata hizo kusoma kata za jirani na kusababisha wanafunzi wengi kutomaliza masomo kutokana na mimba na utoro.

.Mh.Naibu Waziri akizungumza na wananchi wa kata ya Msisima 
.Diwani wa kata ya msisima akimshukuru Naibu waziri kwa kutembelea kata ya Msisima ambayo haijawahi kutembelewa na kiongozi mkubwa ngazi ya kitaifa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...