Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
Wananchi
 wameaswa kushirikiana na TAKUKURU ,kupambana na rushwa na kufichua 
waomba rushwa ambao uomba rushwa wakati wa kutoa huduma mbalimbali za 
kijamii ili waweze kuchukuliwa hatua.
Aidha
 idara na taasisi zinazotoa huduma kwa jamii ikiwemo Jeshi la polisi 
kitengo cha usalama barabarani, hospital zimeelekezwa kukusanya mapato 
kwa njia ya kielektroniki, TEHAMA ili kuongeza pato la Taifa na 
kurahisisha huduma.
Akitoa
 ujumbe wa mwenge wa uhuru kwa wananchi wa Rufiji pamoja na kuzindua  
klabu ya kupambana na rushwa shule ya sekondari Mahege,mkoani Pwani, 
Kiongozi wa mbio za mwenge maalum ,L.T Josephine Mwambashi alisema,  
jamii itambue mapambano hayo sio jukumu la TAKUKURU pekee.
Mwambashi alielezea, rushwa inarudisha nyuma maendeleo.
Hata
 hivyo , akielezea umuhimu wa TEHAMA aliwataka wanafunzi kutumia njia 
hiyo ikiwemo simu, komputa ,Tv kuongeza uelewa na ufahamu wa mambo ya 
masomo lakini sio kwa kumong'onyoa maadili yetu.
Akiweka
 jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji safi katika 
Kijiji cha Nyamisati ,unaosimamiwa  na wakala wa maji na usafi wa 
mazingira vijijini (RUWASA ), Mwambashi alisema wanaosimamia miradi 
wahakikishe wanashirikisha jamii ili itambue.
Mradi
 mwingine ni Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya 
walimu katika shule ya sekondari Zimbwini, Mwambashi alipokea taarifa ya
 mradi iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo Estomic Kimwemwe ambapo 
alielezea ,malengo ya mradi ni kupunguza msongamano wa wanafunzi 
madarasani.
Alisema 
,utekelezaji wa mradi ulianza mei 2021 na ulitarajiwa kukamilika agost 
20 ,mwaka huu fedha zilipokelewa kwa ajili ya Ujenzi zimetumika milioni 
39.662.5 na zimebakia 337,500 .
Awali
 akipokea mbio maalum za mwenge wa uhuru ,kutokea wilayani Rufiji,mkuu 
wa wilaya ya Kibiti ,kanal Ahmed Abbas Ahmed alisema ,mwenge huo 
utatembelea miradi 15 yenye thamani ya sh .474.540.5.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...