Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge 2021 Luteni Josephine Mwambashi amezitaka taasisi za Serikali Nchini  kuwashirikisha wananchi wakati wa utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa mradi wa maji Chalinze Mboga wenye thamani ya Bilioni  17.3

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inatekeleza mradi huo ambapo umefikia asilimia 95 na kufikia Septembea 15 utakuwa umekamilika.

Luteni Mwambashi amesema, ni suala la muhimu kwa wananchi kushirikishwa katika utekelezaji wa miradi hiyo  ili kuwapa uelewa na kufahamu umuhimu wake kabla ya kuanza kuwahudumia.

Amesema,” kuna umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi kuanzja ngazi ya juu hadi chini ili kuwapa ufahamu kuhusu miradi inayotekelezwa katika maeneo yao, gharama za mradi, unaanza lini na kumalizika lini,”

“Nimeona mradi huu wa DAWASA ni mzuri nimeukagua na nawaomba ikifika Mwezi Septemba wananchi waanze kupata huduma ha maji safi kwani maji ni muhimu kwa kila mwananchi,” amesema Luteni Mwambashi.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huo umefikia asilimia 95 na unatarajia kukamilika mwezi Septemba.

Amesema, katika utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa na Dawasa wameshatumia kiasi cha shillingi Bilion 13 na umehusisha ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji (booster station) na pampu na ulazaji wa mabomba kwa Km 59 kutoka Mlandizi hadi Mboga.

“Mradi huu unakamilika Septemba 15 na kuanzia Septemba 20 tutaanza kuwasha pampu za kusukuma maji na kukamilika huko tutaanza kufanya maunganisho kwa wateja wapya,” amesema Luhemeja.

Aidha akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Uwekezaji Dawasa Mhandisi Ramadhan Mtindasi amesema mradi wa Chalinzw Mboga utahudumia zaidi ya kaya 100,000 (laki moja), maeneo ya Viwanda na utazalishaji maji lita Milion 9.5
 
Ameongoza kuwa mradi huo wa Chalinze Mboga utahudumia maeneo mbalimbali
Kwala, Mbala, Chamakweza, Pingo, Msoga, Mboga na vijiji vingine vya karibu.

Mbio za Mwenge kitaifa zinaendelea kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo na Kiongozi wa mbio hizo kutoa maagizo kwa mamlaka na taasisi zinazotekeleza miradi hiyo.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Miradi DAWASA Mhandisi Ramadhan Mtindasi akitoa maelezo ya mradi wa Chalinze Mboga Kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huo uliofanyika leo Mkoani Pwani. Kiongozi wa Mbio za Mwenge amewataka Dawasa kuwashirikisha kwa undani zaidi wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi yao

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi akizindua na kuweka jiwe la msingi la mradi wa Chalinze Mboga wenye thamani ya Bilion 17.3  baada ya kuutembelea na kuukagua. Uwekaji huo wa jiwe la msingi umefanyika leo Mkoani Pwani
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo ya mradi wa Chalinze Mboga Kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi huo uliofanyika leo Mkoani Pwani. Kiongozi wa Mbio za Mwenge amewataka Dawasa kuwashirikisha kwa undani zaidi wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi yao

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Luteni Josephine Mwambashi akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Miradi Mhandisi Ramadhani Mtimdasi baada kutembelea mradi wa Chalinze Mboga wenye thamani ya Bilion 17.3 Uwekaji huo wa jiwe la msingi umefanyika leo Mkoani Pwani
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...