NIMEGUSWA! Ndiyo kauli unayoweza kuitumia baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi kukamilisha ahadi yake kwa mmoja wa wananchi wake ambaye ni mlemavu kwa kumpatia Baiskeli Maalum zinazotumiwa na watu wenye ulemavu.

Kunambi pia ameahidi kumpatia Bati 20 mmoja wa wananchi wake wenye ulemavu ikiwa ni ahadi yake kwake baada ya Mwananchi huyo kuomba msaada huo wakati Mbunge Kunambi alipofanya ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni kwake.

Akizungumza katika kijiji cha Ngalimila Kata ya Utengule ambapo ndipo alipokabidhi baiskeli hiyo amesema alipata barua ya maombi ya baiskeli kutoka kwa Mzazi wa kijana huyo ya kuomba kupatiwa baiskel ambapo wakati wa kukabidhi amewaomba watanzania wote kuwa na utaratibu wa kusaidia watu wenye uhitaji.

"Watanzania sisi tuna moyo wa kipekee hivyo niwaombe tujenge utaratibu wa kusaidia wenzetu wenye uhitaji, kufanya hivi ni kuendeleza moyo wa upendo ambao tuliachiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere lakini pia kupata baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Hivyo leo nakabidhi baiskeli hii kwa Ndugu yetu huyu ili iwe msaada kwake katika shughuli zake za kila siku, lakini kuna mwenzetu mwingine wa Kata ya Kamwene yeye amejenga nyumba yake lakini amekwama Bati, nimuahidi kumletea Bati 20 ndani ya muda mfupi kutoka sasa," Amesema Kunambi.

Akiwa kweye ziara yake Kata ya Kamwene, Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi alikutana na Mwananchi huyu mwenye ulemavu ambapo alimuomba Mbunge huyo kumuwezesha kumalizia Nyumba yake na Kunambi kumuahidi mabati 20 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wake huo.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi amekabidhi baiskeli maalum ya kutembelea watu wenye ulemavu kwa mmoja wa wananchi wake wa Kata ya Utengule ambaye aliomba kusaidiwa baiskeli hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi akiagana na Mwananchi ambaye amemkabidhi baiskeli maalum ya kutembelea Ili kuweza kufanya shughuli zake mbalimbali.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...