Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
WILAYA ya Mafia mkoani Pwani,imepokea chanjo ya UVIKO 19 zipatazo 1,000 ambazo zitasaidia kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Mkuu
wa wilaya hiyo ,Mhandisi Martin Ntemo amepokea chanjo katika uzinduzi
wa utoaji wa chanjo hiyo kiwilaya na kuchanja kwa hiari yake.
Baada
ya kuchanja ,Ntemo alieleza chanjo zilizopolelewa kwa awamu ya kwanza
zitaanza kutolewa kwa wauguzi na watoa huduma wa afya.
Alisema
kwamba,pia watapatiwa watu wenye umri zaidi ya miaka 45 wenye
changamoto ya maradhi ya muda mrefu, watumishi wa umma,wahudumu katika
mahotel na migahawa,na wazee.
Maeneo yatakayotoa huduma hii ni hospital ya wilaya, pamoja na zahanati ya Baleni,Utende,Bweni,Chemchem na Kirongwe.
Ntemo
aliwahamasisha wananchi kujitokeza kuchanja chanjo hiyo itakayowasaidia
na kuwaomba wapuuzi uzushi wowote juu ya chanjo hiyo.
"Licha ya kuwa ni kinga lakini pia itapunguza makali ya homa ya ugonjwa huu na vifo vinavyotokana na Uviko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...