Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Nyota wa Kimataifa wa Argentina, Lionel Messi  amejikuta akibubujikwa na machozi katika mkutano wake wa mwisho wa kuwaaga Wachezaji wenzake wa Barcelona baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 21 tangu ajiunge akiwa na miaka 13.

Messi na FC Barcelona walilazimika kuachana msimu huu kutokana na sababu ya vizuizi vya kifedha na utawala kwa Kanuni za Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga), awali ilielezwa kuwa Messi alikuwa tayari kuongeza mkataba hadi 2026 na Barcelona, mkataba ambao uliokuwa na kipengele cha kupunguza mshahara wake.

Hali hiyo ilitegemea zaidi Barcelona kuuza Wachezaji ili kumudu mshahara wake kipindi akiwepo klabuni hapo. La Liga imesema kuwa klabu lazima ipunguze mshahara kabla ya Messi na Mchezaji yeyote yule mpya kusajiliwa.

Katika Mkutano huo Messi amesema, “Hii ni ngumu, sikujiandaa na hili. Mwaka uliopita walinishauri kuondoka, lakini mwaka huu nimelazimika, Familia yangu na nilitaka kubaki hapa, katika nyumba yetu”.

“Baada ya miaka 21 naondoka hapa nikiwa na Watoto watatu. Tuliishi vizuri katika mji huu, hapa ni nyumbani kwetu, nilifurahi kwa kila kitu, wenzangu na kila mtu aliyekuwa na mimi”.

“Nilijitoa kwa kila kitu katika Klabu hiyo tangu nifike kwa mara ya kwanza na hadi naondoka. Siamini kama nawaaga na sikuwahi kabisa kama nitakuja kuwaaga siku moja, nilifanya kila kitu nibaki Barcelona lakini Kanuni na Sheria za La Liga ilishindikana mimi kubaki hapa”.

Hata hivyo, baada ya kutangaza kuondoka Barcelona, Messi amehusishwa kutimkia katika Klabu ya Paris Saint-Germain wanapochezea Nyota, Neymar Jr, Angel Di Maria na Nyota wengine wengi mashughuli duniani kwa sasa.

Lionel Messi akiwa FC Barcelona amecheza michezo 778 katika mashindano tofuati na kufunga mabao 672 sambamba na kubaba Ballon d'Or kwa rekodi ya mara 6 huku akiikusanyia mataji 34 Klabu hiyo yakiwemo La Liga (10), Ligi ya Mabingwa Ulaya (4) na Copa del Rey msimu wa 2020-2021.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...