Na Farida Saidy Morogoro.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale anashikiliwa na
polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,100 mali ya
halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Muslimu amesema hayo leo
Jumanne Agosti 24, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari
ofisini kwake.
Muslimu
amesema kutokana na wizi huo watu wengine saba wanashikiliwa na
wanadaiwa kushirikiana na Mkurugenzi huyo na wanaendelea kuhojiwa.
Aidha
Kamanda Muslim amesema wizi wa mabati hayo ulifanyika Juni 17, 2021
eneo ya ujenzi kitongoji cha Mvumi B wilayani Kilosa katika stoo ya
halmashauri hiyo ambayo haikuvinjwa ambapo stoo hiyo haikuvunjwa.
Awali Mwambambale alikuwa mkurugenzi wa halmamshari ya Kilosa kabla ya kuhamishwa halmashauri ya Gairo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...