Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

Muanadaaji wa Tamasha la Shukurani, Msama Promotion  Alex Msama ametangaza mabadiliko ya tamasha hilo na kutaja tarehe rasmi ya tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Msama amesema kuwa kilicho badilika katika muendelezo wa maandalizi ya tamasha hilo ni tarehe tuu.

Amesema tamasha lilipangwa kufanyika Oktoba 3,2021 na sasa litafanyika Oktoba 31,2021 katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar es Salaam.

“Mashabiki wakae mkao wa kula kwani tumejipanga vizuri na wasanii mbalimbali wakubwa wakiwemo ndani na nje wataimba live,” alisema Msama.

Msama amesema yeye pamoja na Kampuni yake kwa ujumla wanaahidi kufanya tamasha la kihistoria, kutakuwa na wasanii mbalimbali vikiwemo vipaji vipya vyenye uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo za injili jukwaani.

Hata hivyo Msama ameeleza kuwa tamasha hilo lipo kwa ajili ya kusifu na kuabudu huku burudani ikiwa ni sehemu ya kuwaweka karibu watu wa Mungu kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani ya jiji la Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama promotion, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam na kutaja tarehe rasmi ya kufanyika kwa Tamasha la Shukurani kwa Mwaka huu ,pichani kushoto ni a mwimbaji wa nyimbo za injili Edson Mwasabwite

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...