Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Utunzaji wa mazingira unapaswa kupewa kiupaumbele hasa kwenye vyanzo vya Maji ili kuweza kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi. Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi alipotembelea utunzaji wa chanzo cha maji cha mto Mzinga na kupanda mti. Chanzo hicho kilianza mwaka 1950 ambacho kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita milioni saba hadi tisa kwa siku.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kupanda mti kwenye chanzo cha mto Kizinga amesema DAWASA kwa kushirikiana na wananchi wanapaswa kuwa walinzi bora kwenye kulinda vyanzo vya maji. Kwani vyanzo vya maji vikikauka hakutakuwa na haja ya kuwepo kwa Mamlaka hiyo.
Amesema Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 umeamua kutembelea chanzo cha maji cha mto Mzinga ili kuona uwezo wake wa uzalishaji wa maji pamoja na kuhamasisha upandaji wa miti kwenye vyanzo mbalimbali vya maji kikiwemo cha Mto Kizinga.
Akisoma taarifa ya utunzaji wa chanzo cha maji cha mto Kizinga Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe amesema DAWASA kupitia mtambo wa Mtoni iliweka lengo la kuongeza mtandao wa huduma ya maji ikiwemo kufikisha maji katika Tenki la Mbagala ili kuwafikia watumiaji wapya zaidi 100,000.
Amesema mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2019 zilipata kuzindua zoezi la kupanda miti ili kukitunza chanzo hiki cha maji na kutoa ujumbe wa wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji. Baada ya ujumbe huo kuwafikia wananchi muitikio umekuwa mkubwa na hali ya mto mzinga imezidi kuwa nzuri kwa muda wote hata kipindi cha Kiangazi.
Utunzaji na upandaji wa miti katika chanzo hiki umesaidia kuongezeka kwa wingi wa maji ambayo kwa sasa yamewezesha kuwafikia watumiaji wapya 168,450 ambao hapo awali huduma ilikuwa haijawafikia. DAWASA itaendelea kutoa elimu kwa jamii inayokaa karibu na hifadhi ya mto ili kuhakikisha lengo la Serikali la kumtua mama ndoo ya maji kichwani linafikiwa.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe akitoa ufafanuzi kuhusu namna Mtambo unavyofanya kazi na usambazaji kupitia mchoro kwa Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembea kituo hicho cha kilichopo Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe(wa kwanza kulia) akimuongoza Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi eneo lililoandaliwa kwa ajili ya upandaji wa miti ya Mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2021 katika Chanzo cha maji cha Mto Kizinga Mtamb kilichopo Mtoni Manispaa ya Temeke leo.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akipanda mti katika eneo la Uzalishaji maji wa Mtambo wa Mtoni ili kuendelea kutunza chanzo cha maji cha Mto Kizinga mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea kwenye kituo hicho kikongwa hapa mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akipanda mti katika eneo la Uzalishaji maji wa Mtambo wa Mtoni ili kuendelea kutunza chanzo cha maji cha Mto Kizinga mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea kwenye kituo hicho. Kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi wakisililiza taarifa fupi ya utunzaji wa Chanzo cha maji cha Mto Kizinga iliyokuwa ikisomwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipotembelea Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo cha Mto huo. Kulia ni Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi akitoa hotuba yake kwa wafanyakazi wa DAWASA, Manispaa ya Temeke pamoja na wananchi waliofika kwenye Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo hicho leo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili eneo hilo leo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo wakiwasili na Mwenge wa Uhuru kwenye Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo pamoja na kukagua Maendeleo ya chanzo hicho ambacho ni kikongwe hapa nchini.
Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika Chanzo cha maji cha Mto Kizinga kwa ajili ya kupanda miti ili kutunza chanzo
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe akitoa ufafanuzi kuhusu Chanzo cha maji cha Mto Kizinga wakati wa kukagua chanzo hicho na Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kutembea kituo hicho cha kilichopo Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...