Na Mwaandishi Wetu Mtwara
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Yusuf Nannila amelitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuharakisha taratibu za kupeleka nishati hiyo katika mradi wa maji uliopo katika kata ya Nangomba Wilaya ya Nanyumbu ili kuwezesha wanananchi wa maeneo hayo kupata maji kwa wingi na kwa bei nafuu.
Nannila ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara katika Wilaya ya Nanyumbu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
“Ninaagiza TANESCO kufanya mawasiliano na Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya ili waje haraka kufunga umeme hapa (akiwa kwenye mradi wa maji) ili wananchi wa kata ya Nangomba waweze kupatiwa maji kwa bei nafuu na kwa wingi,” amesema Nannila.
Nannila ametoa maagizo hayo baada ya kuelezwa na Mhandisi wa Maji kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nanyumbu Mchucha Saimon kwamba wananchi wanauziwa maji kwa Sh 100 kwa ndoo.
Mhandisi huyo amesema kwa sasa wanatumia jenereta kupampu maji ambayo yanatumiwa na wananchi jambo ambalo alisema wakala hao wanatumia gharama kubwa kununua mafuta kwa ajili ya jenereta hivyo kuwalazimu kutoza wananchi Sh 100 kwa ndoo ya maji.
Kufuatia hatua hiyo Nannila amewataka RUWASA kupunguza bei ya maji kutoka Sh 100 mpaka 50 ili wananchi waweze kupata maji kwa urahisi na kwa wingi.
Nannila pia ameishukuru serikali kwa kupeleka mradi huo wa maji ambao kwa sasa unawezesha wananchi kupata maji kwa haraka na urahisi.
“Mradi ni mzuri sana ambao unaleta faraja na kuonyesha kwamba utekelezaji wa ilani unakwenda vizuri,” amesema. Kamati hiyo ya siasa Mkoa wa Mtwara ipo kwenye ziara ya siku sita katika mkoa huo kukagua utekelezaji wa ya chama hicho," Amesema Nannila.
Wakiwa katika Wilaya ya Nanyumbu, Kamato hiyo ilitembelea na kukagua miradi ujenzi wa hosteli katika shule ya Nangomba na Likokoma, ujenzi wa madarasa na ukamilishaji wa maabara shule ya Likokoma na ujenzi wa chumba cha mionzi katika hospitali ya Mangaka.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Yusuf Nannila akifungua kiko ya maji katika bomba la maji ambalo lipo katika shule ya sekondari ya Nangomba Wilaya ya Nanyumbu Mkoa Mkoani Mtwara mara baada ya kutembelea mradi wa maji unaotekelezwa na Serikali katika Kata ya Nangomba. Mwenyekiti pamoja na wanakamati wa kamati ya CCM mkoa wa Mtwara walikuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya cham hicho Mkoani humu
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa meneja wa RUWASA Wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Mchucha Saimon (wa pili kushoto) wakati alipotembelea mradi wa maji wa Nangomba Wilaya ya Nanyumbu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...