Makamu wa Rais wa Miss East Africa Beauty Pageant Joyli Mutesi (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano wao na wanahabari kutangaza rasmi kufanyika kwa shindano la Miss East Afica 2021 litakalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwezi Novemba 26 mwaka huu Jijini Dar es salaam. (wa kwanza kulia) ni Rais wa Taasisi hiyo Rena Callist na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko.
Makamu wa Rais wa mashindano ya urembo ya mrembo wa Afrika Mashariki( Miss East Africa Beauty Pageant Joyli Mutesi akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) kwenye mkutano huo.
Rais wa Mashindano ya Urembo kutoka Miss East Africa Beauty Pageant Rena Callist (kulia) akizungumza kuhusu mashindano hayo leo Agosti 31,2021 jijini Dar es Salaam.

Gari mpya aina ya Nissan X Trail ambayo imetangazwa kama zawadi atakayopewa mshindi wa Mashindano ya Miss East Africa ikiwa tayari imeshatangazwa rasmi ikisubiria mshindi wa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MASHINDANO ya Urembo 'Miss East Africa' yanatarajia kufanyika  Novemba 26 mwaka huu ambapo washiriki kutoka nchi 16 wanatarajia kushiriki huku zawadi ya mshindi wa kwanza ikiwa gari mpya aina ya Nissan X Trail toleo la mwaka 2021/21 lenye thamani ya Sh.110,000,000.

Akizungumza leo Agosti 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano ya Urembo kutoka Miss East Africa Beauty Pageant Rena Callist amesema jumla ya zawadi zenye thamani ya Sh.milioni 146 zitatolewa katika mashindano hayo ya mwaka huu.

Callist amefafanua mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atazawadiwa gari jipya la kisasa aina ya Nissan x Trail,toleo la Mwaka 2021/21 lenye thamani ya shilingi 110,000,000, mshindi wa pili atapata fedha Sh.milioni 11 wakati mshindi wa tatu ataibuka na kitita cha Sh.milioni tano.

Aidha kutakuwa na zawadi zingine mbalimbali kwa washiriki wa mashindano hayo zenye thamani ya Sh.milioni 20 huku akisisitiza  jumla ya nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam.

Amezitaja nchi zilizothibisha kushiriki ni Tanzania,Kenya,uganda,Rwanda,Burundi, South Sudan,Ethiopia,Elitrea,Djibouti,Somalia,Malawi,Visiwa vya Seychelles,Comoros,Madagascar,Reunion na Mauritius "Calist amesema.''

Ameongeza mashindano ya Mwaka huu yanatarajiwa kurushwa moja kwa moja na kuangaliwa na watazamaji zaidi ya  milioni  300 kupitia luninga na mitandao ya kijamii duniani  ambapo Tanzania itafaidika na mashindano hayo moja kwa moja kwa kutangaza vivutio vya utalii, fursa za uwekezaji wa biashara na utamaduni kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...