Na Zainab Nyamka,Michuzi TV

SERIKALI imewapongeza Shirika la Posta Tanzania (TPC) na benki ya CRDB kuboresha ushirikiano wao katika kutoa huduma za kifedha kwenye Ofisi 200 za Shirika hilo nchini.

Washirika hao wametakiwa kuhakikisha huduma zao zinawafikia watanzania wengi ili Tanzania ifikie uchumi wa kidigitali.

Akizindua huduma za CRDB wakala katika ofisi za shirika la Posta,  Waziri wa Mahusiano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile amesema fedha ni kichocheo muhimu katika maendeleo hivyo kuna kila sababu ya kutanua wigo wa huduma za kifedha kwa watanzania.

Dk.Ngudulile amesema bado takwimu za matumizi kwenye mfumo rasmi wa huduma za kifedha ni mdogo hivyo mahusiano hayo yahakikishe watanzania wengi zaidi wanaingia kwenye mfumo huo.
 
"Kwenye mfumo rasmi wa huduma za kifedha ni mdogo kwani asilimia 16.7 wanapata huduma za kifedha kupitia benki,asilimia 48.6 wanapata huduma za kifedha kupitia simu za mkononi,asilimia 6.7 haijulikani wanapata huduma kupitia mfumo gani huku asilimia 28 hawana huduma hiyo"amesema Dk.Ngugulile.

Amesema  kuwa mahusiano hayo yawafikie kwa kuwarasimisha watanzania kwenye mfumo rasmi wa fedha.

Dk Ndungulile ameongeza kuwa Serikali imeendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ambapo bajeti ya mwaka 2021/22 imetenga sh. Bilioni 300 kwa ajili ya kuboresha huduma na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali.

Pia amelipongeza shirika hilo kwa kuanzisha huduma ya pamoja (One Stop Centre) ambayo itarahidisha huduma mbalimbali za kiserikali kwa wakati mmoja pamoja na kuanzisha duka mtandao na watanzania kupata fursa ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Naye, Kaimu Posta Masta Mkuu Macrice Mbodo alisema shirika limeazimia kuhudumia wananchi na kuchagiza maendeleo ya kiuchumi.

AmeseMa shirika hilo limeunganisha zaidi ya ofisi 350 nchini pia lipo katika Umoja wa Posta Duniani (UPU)lenye matawi zaidi ya 670,000 duniani.

Mbodo amesema, kuna jumla ya maduka mtandao 270 na yote yanatoa huduma ndani na nje ya nchi na watanzania wananufaika kwa kupata fursa ya kuuza bidhaa zao popote duniani na Shirika la Posta limekuwa linasafarisha bidhaa hizo kwa uaminifu na usalama mkubwa.

Kwa upande wake Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara kutoka shirika hilo Costantine Kasese alisema mbali na kutoa huduma xa kifedha shirika linatoa huduma ya usafirishaji wa barua,vifurushi na sampuli kwa ajili ya kupeleka kwa mkemia.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Sekela amesema atahakikisha mawakala wanafanya kazi kwa ueledi na kuwapatia mafunzo ili kuboresha utendaji kazi wao na wananchi kupata huduma bora.

Majid ameongeza kuwa. walikua na ushirikiano na Shirika la Posta toka 2013 lakini kwa mwaka 2021 wameamua kuboresha zaidi ushirikiano huo kwa kuziunganisha taasisi hizo na kuanza kutoa huduma za kifedha ndani ya Ofisi 200 za Shirika hilo.

“Ubunifu ni jambo la msingi katika kuchagiza ukuaji wa uchumi,
Benki yetu imejikita zaid katika mfumo wa kidijitali na kwa saaa tumeungana na mdau mkubwa ambaye ni Posta kwa sababu yupo nchi nzima na sisi huduma zetu zinazidi kusogea karibu zaidi,” amesema Majid.

Ameongeza kwa kulishukuru Shirika la Posta kwa kuwa na imani nao na amewaahidi kushirikiana nao na wamejiandaa kutoa huduma bora kwa watanzania.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Faustine Ndungulile(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma za kibenki ndani ya Shirika la Posta. Kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo na Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Sekela. Hafla hiyo imefanyika leo katika Makao Makuu ya Shirika La Posta Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Faustine Ndungulile akiwapongeza Shirika la Posta Tanzania na Benki ya CRDB kwa kuboresha ushirikiano wa huduma za kifedha katika ofisi zao na kuwataka ziwafikie watanzania wengi ili Tanzania ifikie uchumi wa Kidigitali.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo akizungumzia ubia walioingia na Benki ya CRDB utakaowawezesha wananchi kuanza kupata huduma za kibenki ndani ya ofisi za Shirika hilo zilizopo kote nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Sekela akitoa maelezo kuhusiana na ushirikiano uliopo kati ya benki hiyo na Shirika la Posta na namna walivyojipanga katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja wote watakaofika ndani ya Ofisi 200 za Shirika hilo kote nchini.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...