Mmoja wa wataalamu akihakiki matokeo ya chunguzi walioufanya mara baada ya kuweka vimelea kwenye incubator ndani ya masaa 48 kujiridhisha kama vilea vilivyotoka katika maji ama chakula ni salama au ni hatari kwa matumizi.Meneja wa Upimaji (TBS), Bw.Joseph Makene akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufanyaji kazi wa maabara za TBS zilizopo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wataalamu akifanya uchunguzi wa maji na kuhakiki kama ni salama kwaajili ya matumizi kwa binadamu.

 

Mmoja wa wataalamu akifanya uchunguzi wa baadhi za sampuli zilizopo katika maabara ya microbilogy (TBS) ili kuweza kupata matokeo uya uchunguzi walioufanya kwenye chakula au maji na kuhakiki usalama wa maji na chakula.  

Mkuu wa Maabara ya Microbiology (TBS), Bw.Salum Kindoli akielezea namna wanavyofanya uchunguzi kwa kuweka sampuli zilizofanyiwa utafiti kwenye incubator ili kupata matokeo ya uchunguzi walioufanya kwenye maji au chakula.

{PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO}

***********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lina jumla ya maabara tisa ambazo zinatumika katika uchunguzi wa bidhaa mbalimbali ambazo ni bora na kuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi pamoja na wataalamu waliobobea katika uchunguzi.

Ameyasema hayo leo Meneja wa Upimaji (TBS), Bw.Joseph Makene wakati akitoa taarifa juu ya ufanyaji kazi wa maabara hizo zilizopo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw.Makene amesema TBS ina maabara za kupima nguo na ngozi, maabara hizo zinatumika katika uchunguzi wa bidhaa zote zinazohusu nguo na ngozi pia kuna maabara za kupima vifaa vya kikemikali ambayo hutumika kupima vipodozi pamoja na bidhaa zote za petroli.

Amesema kuna maabara ya Microbiolojia "Maabara hii inafanya uchunguzi wa uwepo wa vimelea vya magonjwa katika bidhaa zote ambazo zinapatikana nchini". Amesema Bw.Makene.

Aidha Bw.Makene amesema TBS ina maabara tatu za uhandisi ambapo kuna maabara ya uhandisi umeme ambayo inafanya uchunguzi wa vifaa vyote ambavyo vinahusiana na umeme kama vile Tv,simu, kompyuta na vingine vingi.

Amesema kuna maabara ya uhandisi mitambo ambayo inafanya uchunguzi wa bidhaa zote zinazohusu mitambo.

Vilevile amesema kuna maabara ya Ujenzi "Maabara hii inapima bidhaa zote za ujenzi kama mabomba yanayotumika katika kupitisha maji majumbani kwetu na kwenye miradi mbalimbali". Amesema Bw.Makene.

Hata hivyo kuna maabara zingine ambazo ni maabara ya kupima vifungashio na maabara ya ugezi ambayo inafanya ugezi wa vipimo vyote ambavyo vinatumika katika uzalishaji viwandani pamoja na kwenye hospitali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...