Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu anaesimamia dawati la ithibati Bi.Stella Mroso amesema kuwa ithibati inaweza kutolewa kwenye taasisi za upimaji, ukaguzi, uthibiti wa ubora ikiwa na lengo la kujenga imani kwa watumiaji wa bidhaa au huduma kuona inafaa kwa matumizi.
"Ithibati ni nyenzo muhimu katika kuondoa vikwazo vya kibiashara kitu ambacho kitachangia kukuza uchumi wa Taifa letu hasa katika Uchumi wa viiwanda". Amesema Bi.Stella.
Aidha Bi.Stella ameelezea manufaa ya kutekeleza mifumo ya kiwango cha kimataifa katika maabara za upimaji za ugezi ambapo moja ya manufaa ni kujenga imani kwa wateja, kuziwezesha maabara kufafanua na kuainisha kazi zao lakini pia kuweka malengo ya ubora katika kufikia malengo ya taasisi.
Hata hivyo ameelezea ni maandalizi gani kama maabara wanatakiwa kuwa nayo ambapo kabla ya kuomba cheti cha ithibati ya umahili moja ya maandalizi ni kupata uelewa wa matakwa ya viwango husika kwa kupatiwa mafunzo ambayo yanatolewa na TBS, hatua nyingine ni kufuata matakwa ya yaliyowekwa ya kimataifa.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...