Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wamefanya uchaguzi wa viongozi wapya  wa tawi ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano uliofanyika leo katika ukumbi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Nafasi zilizogombaniwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Tawi ,Katibu wa Tawi, Mwenyekiti wa Wanawake, Katibu wa wanawake, Mjumbe wa Vijana, mjumbe wa kundi la watu wenye ulemavu na wajumbe wa Halmashauri ya Tawi.

Awali akifungua mkutano huo, Afisa Tawala Mwandamizi kutoka TCAA, Patrick Vyamana ameupongeza uongozi uliopita wa TUGHE  kwa kazi nzuri walioifanya katika kudumisha mahusiano mazuri kati ya menejimenti na chama hicho na pia amewasihi  wanachama kushiriki katika shughuli za chama Ili chama kiendelee kuwa hai  na kutekeleza majukumu yake.

Vyamana amewaeleza wajumbe waliohudhuria mkutano huo kuzingatia sheria wakati wa uchaguzi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki  ili kuepusha migogoro na kutoa ahadi ya  ushirikiano kwa  uongozi mpya utakaochaguliwa katika kutatua changamoto zilizopo na kuendelea kusisitiza  katika kudumisha mshikamano na kutoa ushirikiano kwa viongozi wapya watakaopatikana.

``Mchakato huu ni huru na wa haki, halali, na wa kidemokrasia  tunahakikisha tunatekeleza jukumu hili, tukizingatia demokrasia  kuepusha migogoro na baada ya uchaguzi tukubali matokeo na tutoe ushirikiano kwa watakaoshinda.``. Amesema  Vyamana.

Kwa upande wa msimamizi wa uchaguzi ambaye ni katibu wa TUGHE Mkoa wa Ilala Bi. Sarah Rwezaula wakati akitangaza matokeo amewapongeza wajumbe wote ambao wamejitokeza kuwania nafasi hizo na kuwataka wanachama kuwapa ushirikiano viongozi wapya.

Katika uchaguzi huo Bi Jackline Ngoda ameibuka kidedea kwenye nafasi ya Uenyekiti wa tawi kwa kupata kura 39, huku nafasi ya Katibu ikichukuliwa Shukuru Mhina ambaye amepata Kura 51. 

Viongozi hawa wapya wa TUGHE ) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Afisa Tawala Mwandamizi kutoka TCAA, Patrick Vyamana akizungumza na wajumbe wa TUGHE tawi la TCAA wakati wa ufunguzi wa  uchaguzi wa viongozi wapya wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  uliofanyika katika ofisi zake zilizopo mkoani Dar es Salaam leo.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Sarah Rwezaula akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  uliofanyika katika ofisi zake zilizopo mkoani Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamis Kisesa aliyemaliza muda wake akisoma risala kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la TCAA uliofanyika katika ofisi zake zilizopo mkoani Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia zoezi la uchaguzi wa viongozi wa TUGHE tawi la TCAA uliofanyika katika ofisi za mamlaka hiyo leo mkoani Dar es Salaam.
Zoezi la Uchaguzi likiendelea
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea
Mwenyekiti Mpya wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Jackline Ngoda akitoa neno la shukrani mara baada ya kuibuka kidedea kwenye uchaguzi huo uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam
Uongozi mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waalikwa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo iliofanyika leo katika ukumbi wa Mamlaka hiyo mkoani Dar es Salaam.
Uongozi wa zamani wa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waalikwa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo iliofanyika leo katika ukumbi wa Mamlaka hiyo mkoani Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...