Na Richard Mwaikenda, Dodoma
WATU wote watakaolala nyumba za wageni (Gesti) Siku ya sensa ya Watu na Makazi watafuatwa huko huko na makarani kuhesabiwa.
Hayo
yamesemwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa wakati wa
mkutano na wadau wa Mkoa wa Dodoma wa kuhamasisha na kutoa elimu juu ya
sensa ya watu na makazi.
"Watu wote watakaokuwa wamelala
siku hiyo Guest, hotelini makarani watakwenda kuwahesabu ikwemo na wale
wote watakao safiri maeneo mbalimbali," amesema Dkt Chuwa.
Amesema
kuwa siku hiyo usiku majira ya saa 6 na dakika moja makarani wa sensa
wataanza kuhesabu kwenye Gesti, mahotelini, stendi na maeneo mengine
yanayohusisha safari.
Aidha, Dkt. Chuwa amesema kuwa
wageni wote kutoka mataifa mbalimbali ambao siku hiyo ya sensa watakuwa
wamelala nchini watahesabiwa na kuchambuliwa baada ya sensa kujua idadi
yao na idadi kamili ya wazawa.
Amesema kuwa,licha ya
sensa hiyo kuhesabu watu wakiwemo wenye aina mbalimbali za ulemavu,
watoto wa mitaani, lakini pia itagusa sekta nyingi kama vile makazi ya
watu zikiwemo nyumba na aina mbalimbali za mifugo.
Mkutano
huo wa wadau ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Mkoa huo, Anthony Mtaka ulihudhuriwa na
Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Wengine ni Kamishna wa
Sensa, Spika mstaafu, Anne Makinda, wabunge wa mkoa huo, wakuu wa
wilaya, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa
mabaraza ya wazee na taasisi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu.
Sensa
WATAKAOLALA GESTI SIKU YA SENSA WATAFUATWA KUHESABIWA itafanyika
Agosti 2022 na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Samia Suluhu
Hassan jijini Dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...