Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam,

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameiagiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ndani ya wiki moja kufanya kikao cha kuwapitisha wadau marekebisho ya Kanuni ya Leseni Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya mwaka 2003 ili kupata maoni yao.

Mheshimiwa Bashungwa ametoa agizo hilo  Agosti 08, 2021 Jijini Dar es Salaam alipofanya kikao na Menejimenti ya taasisi hiyo ya kufuatilia Marekebisho ya Kanuni hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho ya tozo katika maeneo mbalimbali ya biashara yanayotumia kazi za Muziki.

‘’Ndani ya wiki moja kuanzia leo muende kwa wadau mkawapitishe katika kanuni hizi ili nao watoe maoni yao, hili tunatakiwa kulikamilisha kwa haraka ikumbwe kuna maagizo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa tunatakiwa kugawa mirabaha mwezi Disemba ni lazima mkamilishe hili kwa haraka,’’alisema Bashungwa.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Waziri Bashungwa ameitaka COSOTA kuhakikisha inazingatia maoni yote ya wadau  ili kuepuka migogoro wakati kanuni hizo zitakapoanza kutumika. na kwa maeneo hayo niliyowaelekeza kuyafanyia marekebisho mizingatie kwa kuangalia hali ya uchumi na mwenendo wa athari za ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wa Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga katika wasilisho lake la marekebisho ya Kanuni hizo alifafanua kuwa baadhi ya maeneo yamefanyiwa marekebisho kutokana na kuwa na kanuni hiyo  imekuwa yamuda mrefu hivyo gharama zake zimekuwa haziendani na maisha ya sasa.

‘Katika marekebisho ya Kanuni hizi tumezingatia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ikiwa ni pamoja na kushusha gharama chini ya yale mapendekezo ya awali ya wadau hii ni kwa kuzingatia hali ya sasa ya kiuchumi na kuweka mazingira rafiki ya  ambayo yataweza kulipika,’alisema Mwambinga.

Pamoja na hayo nae Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Emmanuel Ishengoma alieleza katika mapendekezo ya marekebisho hayo, yatasaidia kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mirabaha kwa maeneo ambayo awali yalikuwa haya tozwi gharama hizo za matumizi ya kazi za muziki  kama sehemu za kukufanya mazoezi ‘gym’

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...