Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kesi
za utelekezaji,ulawiti,ubakaji na unyanyasaji wa kingono umetajwa
kuongeza kiwango cha ukatili katika halmashauri ya wilaya ya Njombe hadi
kufikisha matukio ya ukatili wa kijinsia 161 katika kipindi cha miaka
miwili ya 2019/2020 na 2020/2021.
Taarifa
hiyo imebainishwa na afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya
Njombe Avelino Chaula kabla ya mkutano wa baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mtwango
na kulazimika kutoa elimu kwa madiwani na wajumbe wa baraza hilo juu
ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa madiwani na maofisa watendaji wa kata
na kwamba katika matukio hayo yote lakini matukio ya utelekezaji
yameripotiwa mengi zaidi kuliko mengine.
“Kwa
miaka miwili tuna matukio 161 lakini matukio yanayoongoza kwa wingi ni
ya utelekezaji na ukiangalia matukio ya utelekezaji kwa mwaka wa kwanza
tuna matukio 42,na mwaka wa fedha 2020,2021 tuna matukio 57 na haya ni
kwa yale yaliyotufikia ofisini sasa tujiulize ni mangapi
hayajafika?tuombe wazazi wawajibike kulea watoto”alisema Chaula
Kutokana
na hali hiyo baadhi ya madiwani wa kata mbalimbali akiwemo Neema
Mbanga, Isaya Myamba na Roida Wandelage wametaka kuwekwa kwa mikakati
maalumu ya kushughulikia changamoto za ukatili ikiwemo tatizo la kesi
nyingi za ujauzito wa watoto kutomalizika.
“Watoto
wengi wanapita mimba lakini ukianza kufuatilia unaona tu imeishia
hewani kwa hiyo ninaomba halmashauri tuweze kuwa makini na kuyafuatilia
haya kwa nguvu zote”alisema Neema Mbanga
“Nadhani
kuna sababu ya msingi ya kujipanga upya namna ya kudhibiti na
kushughulikia kesi hizi kuhakikisha zinaisha”Alisema Isaya Myamba
Naye
Roida Wandelage alisema “Mtaani kuna kawaida ya kusema kipi bora
nimfunge yule ambaye amempa mtoto mimba au nimuache anilelee mtoto wangu
na haya wanayafahamu”
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe George Makacha ambaye ni
mwanasheria na Valentino Hongoli ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri
hiyo wamewataka madiwani na maofisa watendaji kuitumia mikutano yao ya
hadhara kuhakikisha wanatoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika
jamii.
“Sheria inataka
kama motto amepewa mimba lazima sheria zichukuliwe na sisi kama viongozi
ni vema tutoe elimu zaidi ili wazazi waelimike na kuona uchungu juu ya
watoto”alisema George Makacha
Valentino
Hongoli alisema “Wakati mwingine sisi wenyewe tukijitathmini utakuta
viongozi,watendaji na baadhi ya wananchi wanaonekana kioo kwenye jamii
utakuta ni watelekezaji”
Katika
ripoti ya afisa ustawi wa jamii halmashauri hiyo kwa upande wa
wanafunzi waliopata ujauzito ni 16 kwa mwaka 2020 na 18 kwa mwaka 2021.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino hongoli wakati
wa semina kwa viongozi na wajumbe wa baraza la madiwani akitoa wito kwa
viongozi kuwa wakanza kupambana na vitendo vya ukatili ambavyo kwa kiasi
kikubwa vimekuwa vikifanywa katika wilaya hiyo.Afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Njombe Avelino Chaula
katika semina fupi kwa madiwani na viongozi akieleza idadi ya kesi
zilizolipotiwa ndani ya wilaya hiyo zinazohusiana na maswala ya ukatili :Baadhi ya wajumbe wa semina juu ya maswala ya ukatili na watoto
wakimsikiliza afisa ustawi wa jamii akifundisha namna watoto
wanavyotakiwa kulindwa pamoja kupambana na matendo ya ukatili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...