Na Mwamvua Mwinyi,Pwani


SERIKALI kupitia wizara ya michezo pamoja na TFF imetakiwa kuangalia namna ya kuinua suala la michezo makazini na kuandaa ligi maalum kati ya watumishi wa Umma.

Akizungumza katika mechi ya kirafiki baina ya TANROADS HQ (makao makuu )na TANROADS -Pwani , katika bonanza lililoandaliwa na TANROADS Pwani ,mratibu wa bonanza hilo ,Charles Ndyelabula alisema ,hatua hiyo itasaidia kuibua vipaji vilivyojificha makazini.

"Michezo hii inatuweka imara kufanya kazi ,mtumishi unakuwa na molari wa kutenda kazi kwa bidii na afya inaimarika, Hata hii Corona wakati tunachoma chanjo lakini pia tupende michezo inatupa afya njema"alifafanua Charles.

Katika mechi hiyo ,timu hizo zilitoka sare wakitoka wote suluhu ya bila bila.

Mchezaji wa HQ , Twahir Salim alieleza walijiandaa na kupata nafasi nyingi za wazi lakini hawakufanikiwa kushinda.

"Rais ,wizara ya michezo wangesisitiza michezo hii ,leo imenifunza kuwa inajenga mahusiano ,tunajuana na kubadilishana mawazo ,tumefurahi ,Kifupi Tumeenjoy"!alisisitiza Salim.

Kwa upande wake ,Asosa Mwanilwa ambae ni captain wa timu ya TANROADS Pwani ,alisema wamekubaliana na matokeo kwakuwa pande zote wamejitahidi.

Alisema ,kiukweli timu ya makao makuu ipo imara wanaonekana kuwa na mazoezi ya kutosha hivyo wamejifunza ,sio kusubiri mabonanza ndipo wacheze bali kila siku ni ya mazoezi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...