Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Pamela O’Donnell yailiyofanyika katika Ofisi ya Wizara jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Pamela O’Donnell wakijadili jambo walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma.

Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Pamela O’Donnell akielezea jambo kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine.

Mazungumzo yakiendelea

****************************

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine, leo terehe 1 Septemba 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Pamela O’Donnell Balozi wa Canada nchini Tanzania, yaliyofanyika jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Balozi Sokoine na Balozi Pamela O’Donnell wamejadili masuala mbalimbali muhimu katika kudumisha na kuboresha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano katika masuala ya uchumi baina ya Tanzania na Canada. Kwa kipindi cha takribani miongo sita mahusiano ya Tanzania na Canada yamejikita katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kama vile maendeleo ya viwanda, afya, kuendeleza rasilimali watu, ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa mazingira.

Tanzania ilianzisha mahusiano ya kidiplomasia na Canada mwaka 1961 mara baada ya uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...