Baadhi ya makundi mbalimbali na Viongozi wa Taasisi ya Nipe Fagio wakichambua aina mbalimbali za takataka katika maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Septemba 18.


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

JAMII ya Watanzania imeaswa kuendeleza desturi ya kufanya usafi na kutunza mazingira ili kulinda afya na kuondokana na magonjwa mbalimbali yatokanayo na uchafuzi wa mazingira yanayotuzunguka.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Jamii, Taasisi ya Nipe Fagio, Abdallah Mikulu katika siku ya Usafi duniani, iliyoadhimishwa na Taasisi hiyo Manispaa ya Ubungo ikijumuika na Taasisi zisizo za Kiserikali, Serikali ya Mtaa Ubungo Kisiwani.

Mikulu amesema Taasisi ya Nipe Fagio imeadhimisha siku hiyo katika eneo hilo la Ubungo-Kisiwani ikiwa lengo kubwa la kuhamasisha, kuelimisha jamii kuhusu usafi wa mazingira na umuhimu wake katika utunzaji, uhifadhi.

“Siku ya Usafi duniani, leo tumefanya usafi hapa Ubungo Visiwani, tumehusisha makundi mbalimbali na Taasisi mbalimbali ili kuangalia namna ya ubadilishaji wa Sera za Usafi wa Mazingira, kutoa elimu na uwajibikaji wa Kampuni yanayohusika na uchafuzi wa mazingira”, amesema Mikulu.

Kwa upande wake, Mdau wa Mazingira kutoka Taasisi ya Tanzania Heritage Initiative (TAHI), Nickson Mahenge ameeleza umuhimu wa usafi wa mazingira katika kuleta Afya ya akili na kuleta ufanisi katika kufanya kazi vizuri ambayo husaidia kujenga taifa.

Naye, Godfrey Mroso kutoka Mpango wa Youth Resort, amesema suala la usafi na utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mtu katika jamii, amesema Jamii hususani Vijana ni wadau wakubwa katika kuleta Maendeleo Endelevu kufikia mwaka 2030 kupitia utunzaji wa mazingira na Maliasili.

Siku ya Usafi Duniani huadhimishwa kila mwaka Septemba 18.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...