Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

JUKWAA la Wanawake Wilaya Mkuranga mkoani Pwani wamemchagua Mariam Ulega kuwa Mwenyekiti wao baada ya kuibuka na ushindi wa kura 99 dhidi ya kura saba alizopata mshindani wake.

Akizungumza baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo,Mariam Ulega ameahidi kufanya kazi za kwa bidii,juhudi na maarifa na kwamba hatawaangusha wanawake wa Mkuranga.

"Nitahakikisha nashirikiana  wananchi wote wa Mkuranga katika kuendelea kuleta maendelo .Nitahakikisha nasimama imara katika kuifanya Wilaya yetu inapaa kimaendeleo,"amesema Mariam Ulega.

Amewaomba wanaweke ambao hawana vikundi  wavianzishe na kisha wavisajali na hatimaye kukopeshwa fedha ambazo hazina riba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, na hivyo wataweza kuinuka kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali.

Mbali ya kutoa shukrani kwa wapiga kura wa jukwaa hilo,Mwenyekiti huyo amesema Jukwaa hilo la Wanawake Mkuranga wamepokea Cherahani saba kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega.

"Leo tumepolea Cherehani saba kutoka kwa Mbunge , ni vema  tuzitunze  na zifanye kazi iliyokusudiwa ya kushona nguo za watoto wa shule , uwepo wa Cherehani hizo zitawezesha wakina mama wa Mkuranga tusonge mbele,"amesema.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega  akizungumza na wapigakura baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii,juhudi na maarifa na kwamba hatawaangusha wanawake wa Mkuranga.Uchanguzi  huo umefanyika leo  kwenye ukumbi wa Parapanda  Wilaya ya  Mkuranga Mkoani wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega (kushoto) akimkabidhi Cherehani Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo.

Wanawake wakishangilia  ushindi wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega kama wana  wanavyoonekana pichani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)

Sehemu ya wapiga kura  wakiburudika katika Ukumbi wa  Parapanda  Wilaya ya  Mkuranga Mkoani wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega  (wapili kushoto) akiwa kwenye picha ya mamoja na wapikura.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani,Mariam Ulega(katikati)akipongezwa na wapiga kura.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...