IMEELEZWA  kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa sio waaminifu ,wanapojua wamelimbikiza madeni ya ada, katika shule wanashindwa kulipa na kinachofanyika ni kuwatoa watoto wao katika shule husika na kuwapeleka shule zingine bira kufuata utaratibu.

Kutolipwa kwa madeni hayo kunachangia kurudisha nyuma mapato ya shule.

Hayo yalisemwa na Bahati Dickison ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya awali na msingi Ebonite,katika magari ya wahitimu wa elimu ya awali na msingi.

" Shule yetu inatoa elimu bora ,lakini baadhi ya wazazi pamoja na watoto wao kupatiwa elimu bora,baadhi yao wazazi wameshindwa kulipa madeni ya ada,wamewahamisha watoto wao bira kufuata taratibu  za uhamisho," alisema.

Mwalimu Bahati alisema kuwa, shule yao ina maktaba ambayo imekuwa ni mkombozi kwa wanafunzi kwa kuwa inawasaidia wanafunzi kujifunza kusoma na kuandika.

Alisema kutokana na shule yao kutoa elimu bora ikiwamo na kufanya vizuri katika mitihani ya taifa kila mwaka idadi ya wanafunzi imezidi kuongezeka katika  shule hiyo.

Alisema shule yao pamoja na kuwa inatoa elimu ya awali na msingi,pia ina chuo Cha ualimu ambapo na kozi za elimu maalumu inatolewa.

Aliongeza kuwa shule IPO chini ya chuo Cha ualimu Cha Ebonite.

Alisema mwaka 2015 umepata usajili ambapo ilianza na watoto 66 kwa Sasa inawatoto 225 ambapo wanaume 114 na wasichana 111.

Anasema ongezeko la watoto  katika shule hiyo inatokana na huduma za ufundishaji.

Alisema katika mahafari hayo kwa wanafunzi wa darasa lasaba maafari hayo yanakuwa ya tatu huku kwa wale wa elimu ya awali yanakuwa maafari ya sita.

 Alisema wamewaandaa watoto wao ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.

Pia alisema shule yao imewalea watoto katika maadili mema.ili waendako katika shule zingine wawe na maadili mema.

Alisema wazazi wawaendeleze kielimu watoto wao na wasiishie katika elimu ya msingi pekee.

Mwalimu huyo aliwataka wazazi  kuwa na mipaka katika masuala ya teknolojia ili kuwanusuru watoto wao.

Akizungumza masuala Covid-19 alisema kuwa katika kujilinda wanafuata taratibu za kiafya ikiwamo na kuchukuwa taadhari ambapo kila mwanafunzi mmoja analala katika kitanda  chake pekeyake.

Afisa elimu taaluma Manispaa ya Ubungo, Abdallah Buheti ,ambaye alikuwa mgeni rasim katika mahafari hayo alikiri kupokea malalamiko katika  shule za binafsi juu ya Wazazi kuwahamisha watoto bira kulipa madeni ya ada katika shule walizotoka.

"Taarifa nazipata za wazazi kuhamisha watoto bira kulipa  ada , tatizo hilo kwa sasa halitajitokeza tumetoa passwed kwa walimu wakuu mtoto anapohamishwa taratibu zitafuatwa baina ya Mwalimu mkuu wa shule atokayo mtoto na shule aendayo mtoto,  hapo mzazi hawezi kukwepa ulipaji wa ada anayodaiwa,," alisema.

Alisema uwepo wa shule binafsi ni faida kubwa kwa serikali kutokana na wao kujifunza vitu mbalimbali kupitia shule hizo na hali hiyo imechangia shule za serikali  kuboresha miundombinu yake ikiwamo na kuongeza  ongezeko la ufaulu.

Pia alisema shule ya Ebonite ni moja ya shule zinazofanya vizuri mitihani yake ya kitaifa  katika Manispaa ya Ubungo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...