Mbunge wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi yake ya Asia Foundation kwa ajili yakusaidia jamii ya wafugaji, wakulima na wajasiriamali mbalimbali wa eneo Manyara.
Na Mwandishi wetu, Hanang'
MBUNGE wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga, ameanzisha taasisi yake ya Asia Foundation kwa ajili yakusaidia jamii ya wafugaji, wakulima na wajasiriamali mbalimbali wa eneo hilo.
Halamga amesema lengo la taasisi hiyo ni kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kuwalipia ada wasichana wasiokuwa na uwezo wa kulipa elimu ya sekondari ya juu.
Amesema anatamani kuwasaidia watoto wa kike waliotoka kwenye familia duni wanaofaulu kuanzia kidato cha tano na cha sita wasio na uwezo wa kulipia ada ili wahitimu vyema masomo yao.
Amesema taasisi yake hiyo ina lengo la kusaidia jamii za pembezoni kwa namna moja au nyingine ili kuhakikisha wanapiga hatua kwenye suala zima la maendeleo.
“Ninapambana kwa hata kidogo nilichokipata ili kuweza kubadilisha jamii yangu kwa kuwarudishia kwao ninachopata na wenyewe wapige hatua ya maendeleo,” amesema Halamga.
Amesema lengo lake ni wasichana wa Manyara, waweze kupiga hatua ya maendeleo na kumzidi hata yeye ambaye ni mbunge wa vijana Taifa aliyechaguliwa na vijana wa nchi nzima.
Amesema kabla ya kufikia kwenye kuwalipia ada wasichana hao wa kidato cha tano na cha sita wasiokuwa na uwezo ataanza kwa kuwapa misaada ya kuwanunulia taulo za kike.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...