Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

KINYANG'ANYIRO cha Shindano la kumsaka mlimbwende atakayewania taji la Miss Pwani kwa mwaka huu linatarajia kufanyika Septemba 3 Wilayani Kibaha ambapo jumla ya washiriki 15 kutoka maeneo mbalimbali watapanda jukwaani, huku kila mmoja ametamba kuibuka Mshindi wa kwanza.

Akizungumza na Michuzi Tv,Mratibu wa Shindano Hilo Maryam Ahmed amesema warembo wanaendelea kujifunza na kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana mkoani pwani.

Hata hivyo Maryam ameeleza kuwa Shindano la mwaka huu litakuwa gumu kutokana na uzuri warembo hao kukidhi vigezo vyote.

"Majaji watakuwa na mtihani mkubwa wa kuchagua mshindi, maana warembo wote wana vigezo inavyohitajika"

Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo kushuhudia mshindi atakayepatikana.

"Nitahakikisha mshindi anayepatikana anaingia fainali ya Miss Tanzania , hii ni moja ya malengo yangu"


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...