*Asisitiza Serikali kuendelea kukuza uchumi wa wananchi


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mradi wa kuzalisha umeme wa kikanda wa Rusumo utakuwa mkombozi kwa wananchi wa mikoa ya Kagera, Kigoma , Rukwa na Katavi kwani utazalisha umeme wa uhakika utakaowezesha Mikoa hiyo kuunganishwa na gridi ya taifa.

Mradi huo unaotekelezwa kwa kuzingatia makubaliano ya Kiserikali ya nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi baada ya kuingia makubaliano rasmi mwaka 2012 na utazalisha Megawati 80 ambao kila Nchi mwanachama atapata Megawati 27.

Ameyasema hayo jana (Jumapili, Septemba 19, 2021) baada ya kukagua mradi huo wa uzalishaji wa umeme ulioko katika eneo Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa gharama ya shilingi bilioni 82.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa wakandarasi na wasimamizi wa mradi huo ambao hadi kufikia mwezi Julai, utekelezaji wa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 81.2 ya utekelezaji kuongeza kasi katika ujenzi na kuepuka vikwazo ambavyo awali vilisababisha mradi huo kukamilika kwa wakati. “Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais ninapenda kutoa shukrani kwa wakandarasi na wasimamizi wote wa mradi huu”.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu akizungumza na wananchi baada ya kukagua ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichopo wilayani Karagwe, amesema mkakati wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuboresha na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, hivyo kila Mtanzania afanye kazi kwa bidii.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato (wa pili kushoto) kuhusu handaki la kuchepusha maji wakati alipotembelea Mradi wa Umeme wa Rusumo wilayani Ngara , Septemba 19, 2021. Mradi huo utakaozalisha umeme kwa kutumia maji unagharimiwa na nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato (kushoto) kuhusu ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Rusumo wilayani Ngara, Septemba 19, 2021. Wa tatu kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. Mradi huo utakaozalisha umeme kwa kutumia maji unagharimiwa na nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato (kushoto) kuhusu ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Rusumo wilayani Ngara, Septemba 19, 2021. Mradi huo utakaozalisha umeme kwa kutumia maji unagharimiwa na nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda( (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...