JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Msaidizi wa kazi za ndani (House Girl) jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka (13) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka minne aliyejulikana kwa jina la Natalia Essau.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo mtoto huyo amefariki dunia Septemba 17,2021 saa 09:00 mchana katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru katika halmashauri ya jiji la Arusha wakati akipatiwa matibabu baada ya kupigwa na House Girl.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha kifo cha mtoto huyo mwenye umri wa miaka minne ni baada ya kupigwa na msaidizi wa kazi za ndani (House girl) jina limehifadhiwa mwenye umri wa miaka (13) Mkazi wa moshono ambaye taarifa zimebaini miezi kadhaa iliyopita binti huyo aliajiriwa akitokea Mikoa ya Kanda ya Ziwa kuja Arusha kufanya kazi za usaidizi wa ndani",ameeleza Kamanda Masajo.

Amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi.

Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...