Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Mheshimiwa Christina Mndeme amemaliza ziara yake katika wilaya ya Ruangwa ikiwa sehemu ya Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama hicho pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Lindi.

Ziara hiyo yenye lengo la kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 -2025 imekuwa na mafanikio makubwa sana.

Akiwa wilayani Ruangwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) alitembelea Mradi wa Maji Nandeje uliotekelezwa kwa mfumo wa force account na wenye uwezo wa kuhudumia wakazi 1000.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM ametoa maagizo kwa Wakala Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kujenga vituo zaidi vya maji kijijini hapo kwani kituo kimoja hakitoshi.

“Umetujengea kiosk kimoja hiki hakitoshi kwa watu wa Nandenje, tuongeze viosk vingine”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa amesema wamepokea maelekezo ya Serikali na kusitokee kusimamishwa kwa mradi wowote wa Serikali kusimamishwa kwa sababu ya huduma ya maji kutolipiwa.

Mradi huo wa maji ambao awali Serikali ilitoa fedha shilingi 54,345,762.50 lakini zilizotumika ni shilingi 39,042,905.22 ikiwa sawa na asilimia 71.84% ya fedha zilitotengwa.

Naibu Katibu Mkuu pia alipata nafasi ya kutembelea ujenzi wa shule ya Sekondari Mandarawe, Vijana 23 wa CCM wenye mradi mzuri wa kufyatua matofali na kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa mpira wa Majaliwa Stadium.

Mwisho Naibu Katibu Mkuu alikutana na kufanya Vikao na Wenyeviti wa Mashina ambapo alihimiza kuongeza wanachama, kufanya vikao na kuwajibu wapinzani wenye nia mbaya kwa hoja za msingi ili kuepusha kuenea kwa upotoshaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...