Naibu Spika wa Baraya la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma akizindua kitabu cha muongozo wa Chama cha Tanzania Girl  Guides (TGGA) wakati wa kufunga Kambi ya Mafunzo Elekezi kwa  Viongozi wapya wa chama hicho katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi, mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo ya siku 6 yalianza Septemba 12 na kumalizika Septemba 17,2021. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Maembe na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Spika Mgeni ametoa wito kwa Skauti wa Kike na wanawake kwa ujumla kushikamana kwa kuchapa kazi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika harakati ya kuhakikisha Tanzania inapiga hatua za kimaendeleo.

Katika hafla hizo mgeni rasmi huzo aliwaapisha viongozi wapya zaidi ya 150 kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini TGGA,  akihutubia wakati wa kufunga kambi hiyo. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/ kuona  kupitia clip hii ya video  ujue yalizojiri katika hafla hiyo ya kufunga kambi.....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...