TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yahairishaa shughuli za uchaguzi katika kata ya Kagera Nkanda. Hatua hiyo inatokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma tarehe Agosti 20, 2021 juu ya maombi ya Diwani wa Kata hiyo ya Kagera Nkanda.
Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 13, 2021 na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles imeeleza kuwa katika kikao chake cha tarehe 13 Septemba, 2021, imezingatia uamuzi huo na kwa mamlaka iliyonayo chini ya kifungu cha 41(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura 292, imeamua kuahirisha shughuli za uchaguzi katika Kata ya Kagera Nkanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.
Aidha, shughuli za uchaguzi mdogo katika majimbo mawili ya Konde, Pemba na Ushetu, Shinyanga pamoja na kata 9 zilizopo katika halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara zitaendelea kama zilivyopangwa awali na Tume.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...