Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amos Makala leo September 1, 2021 amewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari zinazopatikana katika jimbo la segerea na majimbo mengine yaliopo Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha wanawaondoa wafanya biashara wote wanaofanya biashara holela pembezoni mwa shule ameeleza hayo akiwa katika ziara maalumu inaolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Jimbo la Segerea wananchi mbalimbali waliudhuria mkutano huo, mkutano huu ikiwa ni mfululizo wa usikilizaji kero kwa Mkoa wa Dar es salaam, Jimbo la segerea lipo katika wilaya ya Ilala ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
Suala la ufanyaji wa biashara kando ya maeneo ya shule ya Buguruni Kisiwani imekua kero kubwa katika Jimbo la Segerea na hata maeneo mengine kwani wananchi wamewasilisha kero hiyo baada ya kuona vibanda vya kufanyia biashara kuongezeka kuzunguka maeneo shule hii ikipelekea uchafuzi wa mazingira, vishawishi kwa wanafunzi Pamoja na kupungua kwa ulinzi na usalama kwa wanafunzi na mali za shule kwa ujumla.
Akitatua kero hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makala amesema “ili naomba niliseme mimi mimi sijaridhishwa na hali hii katika shule zetu kwani hata shule ya msingi Bunge wafanya biashara, wanafanya biashara mpaka getini mwa shule hiyo mpaka mabanda yameizunguka shule hii inahatarisha usalama na kuwarubuni watoto wetu”.
Sambamba na hilo mkuu wa Mkoa amewaagiza wafanya biashara wote wanaofanya biashara pembezeni mwa barabara ikiwemo maeneo ya air port,msimbazi karia koo pembezoni mwa barabara za mwendo kasi, kivukoni Pamoja na maeneo mengine ambayo sio rasmi kwa ajili ya ufanyaji wa biashara waweze kuondoka.“ukiona bango limeandikwa usifanye biashara hapa mfuate mkuu wa wilaya muulize baada ya bango hili hapa sisi tunaenda kufanyia biashara wapi? Yeye atawaelekeza kwani foleni zingine zinasababishwa na ufanyaji biashara holela na hata njia za watembea kwa mguu hufungwa ambapo wanasababisha ajali wakati mwingine hivyo nawaagiza wakuu wote wa shule za msingi na sekondari watu wanaofanya biashara hapo za kujenga mabanda holela hapana,tuwaratibu watu watakaotoa huduma kwa Watoto wetu watu hao wawewanatambulika na shule husika naomba agizo litekelezwe ili kulinda usalama kwa Watoto wetu .”
Aidha,Mkuu wa Mkoa ameendelea kusema “Namuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salam Pamoja na uongozi wake kuhakikisha shule ambazo hazina uzio zinajengewa uzio ili kuondoa adha hiyo na kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi na mali za shule kwa ujumla”.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri wa Jiji la Dar es salaam Bi.Tabu Shaibu amemwakikishia kwamba kwa shule zote ambazo hazina uzio wataanza kujenga punde tu baada ya kukamilisha ujenzi wa madarasa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza na Wakazi wa Jimbo la Segerea leoBaadhi ya Wakazi wa Jimbo la Segerea wakiwasilisha kero Zao kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...