Humphrey Shao,Michuzi Tv

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala leo September 1, 2021 amesimamisha michango yote wanaotozwa wanafuunzi wa shule za msingi na sekondari mpaka pale ambapo utaratibu utakapo fuatwa wa wananchi wenyewe kushirikishwa ili ije kama maombi tuidhinishe”. 

 Aidha RC Makalla ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea kero za Wananchi kwenye Mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo la Segerea ambao Wazazi wamedai wamekuwa wakichangia kiasi Cha  Shilingi 300 hadi Tsh 1,000 kwaajili ya gharama za uchapaji wa mitihani pamoja na masomo ya ziada ambayo ni  kinyume na waraka wa Elimu bure ambapo imeonekana wazazi na walezi kushindwa kuhimili michango hiyo

Vilevile, RC Makalla amesisitiza kuwa kuwe na maridhiano baina ya  wazazi na walimu juu ya michango inayotolewa shuleni endapo wakiridhia michango hiyo watume maombi kwa ofisi za mkuu wa wilaya ili ziweze kuidhinisha michango hiyo."Kama wazazi au walezi wamekubaliana na walimu na kuitishwa mkutano  wazazi hao wanatakiwa kuorodhesha majina yao Pamoja na kuweka sahihi kwamba wamekubali Watoto wao  wasome masome ya ziada au wale chakula cha shule tuko tayari barua hizo zinakuja na zipitie kwa Mkuu wa Wilaya ili ziweze kunifikia na mimi nitapitisha na hata kama ni mradi wananchi washirikishwe na mimi nitaizinisha ili mradi uendelee kusudi tuepushe kero ndogondogo zinazojitokeza baina yetu na wananchi wetu."

Aidha, RC.Makala ameelekeza kuwa kwakua kuna uhaba wa ardhi katika maeneo mengi ya Shule hivyo fedha zinazotolewa kwaajili ya ujenzi wa madarasa zitumike kujenga madarasa ya juu  kusudi  eneo dogo liweze kujanga madarasa yakutosha ."Tumeamua fedha zote zinazotolewa kwaajili ya mradi wa  ujenzi wa Shule zitumike kujenga madarasa ya juu ili tutumie eneo dogo ambalo litaweza kutoa madarasa mengi na yatakayowatosha wanafunzi wengi  zaidi  hayo ndio maelekezo yangu kwa Ofisi ya Mkurugenzi".

Naye Afisa elimu takwimu na vielelezo Bi.Wema Kajigili ameahidi kutekeleza yote walioagizwa kuyafanya ikiwemo suala zima la kusitisha michango kwa wanafunzi  hadi utaratibu mwingine utakapotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza na Wananchi wa jimbo la Segerea katika Mkutano wa Wananchi uliofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Buguruni Ghana 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...