Charles James, Michuzi TV
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imetakiwa kuangalia namna ya kuwakopesha Wanawake Wajasiriamali ili kuepusha kwenda kuchukua mikopo umiza ambayo hupelekea kuporwa mali zao ikiwemo vyombo vya ndani pindi wanaposhindwa kurejesha mikopo hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akifungua Kongamano la Wanawake Wajasiriamali na wasio Wajasiriamali la kukuza uchumi wa taifa, Lililoandaliwa na TCB Bank Jijini Dodoma.
Mtaka amesema Watu wa Benki wanapaswa kujitathimini vizuri na kutafuta chanzo kwanini wanawake wengi na jamii huchukua mikopo umiza ambayo inariba kubwa badala ya kukopa Benki ambako kuna usalama katika mikopo.
“TCB Benki mnapaswa kuliangalia hilo angalie kule wanafanya nini ilinyie mtumie nafasi hiyo kuwakamata wateja wa mikopo Umiza waje wakope kwenye Benki yenu,”amesema Mtaka.
Ameendelea kusisitiza kwa kuutaka uongozi wa Benki hiyo kuchunguza ili kujua wale wanafanya kitu gani ili nao wayafanyie kazi lengo ikiwa ni kuwakamata wateja hususani Wanawake .
“Mkifanya uchunguzi wakujua nini wale wa mikopo ya pembeni wanafanya mtafanikiwa kuchukua wateja wote,na hapo sasa ndio mtaonyesha nini
maana ya kuichukua Benki ya wanawake kwa sababu mtakuwa mnawasaidia mikopo,”amesema Mtaka.
Pia amesema TCB inapaswa kuangalia fursa za miradi iliyopo serikali ukiwemo mradi wa SGR,Bomba la Mafuta na migine ili kuwakopesha fedha wanawake waende kupata nafasi za kuendesha biashara katika miradi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Benki Sabasaba Mashingi amesema lengo la kongamano hilo ni pamoja na kutaka kuwasaidia wanawake kukua kiuchumi,ikiwemo kukuza uchumi wa taifa.
Amesema wao kama Benki wanawathamini sana wanawake,kwa sababu asilimia 50 ya wateja wao ni wanawake,hivyo ndio maana wameandaa Kongamano hiloili kupeana mbinu za kuhakikisha wanawake wanainuka kiuchumi na kukuza uchumi wa taifa.
'' Wanawake ni jeshi kubwa hivyo wajitokeze katika kongamano hilo kuhakikisha wanakuwa karibu na TCB Benki ili waweze kujiendeleza kiuchumi kutokana na ujasiriamali wanaoufanya,''Ameeleza Mtaka.
Amesema yale yaliyosemwa na Mkuu wa Mkoa wao kama Benki watakaa nakuona nini wafanye ili wazidi kuwakusanya wanawake katika Benki hiyo kupata mikopo na kujiinua kiuchumi.
Naye mjasiriamali Rosemary Haule amesema anaishukuru TCB Benki kwa sababu imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mikopo inatoka kwa wakati ambayo inawasaidia katika kuendeleza biashara zao za kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza na mmoja wa Wanawake wajasiriamali waliojitokeza kwenye kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Benki ya TCB jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...