Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya ameagiza halmashauri zote 6 za mkoa huo kuhakikisha zinawaingiza wazee wote wanaostahili kwenye mfumo wa matibabu bure na kupewa vitambulisho vyao vya uzee kabla ya mwisho wa mwezi wa kumi.

Rubirya ametoa agizo hilo wakati akizindua baraza la wazee wa mkoa wa Njombe lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo.

“Naziagiza halmashauri zote kuhakikisha wazee wote wenye stahili wanaingizwa kwenye mfumo wa matibabu bure na wanapewa vitambulisho vyao kabla ya mwisho wa mwezi wa kumi mwaka huu.Ninawaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha wanasimamia hili”alise Rubirya

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema mpaka sasa katika mkoa wa Njombe ni wazee 13,100 pekee wasio kuwa na uwezo ndio waliopatiwa vitambulisho vya uzee.

“Nimefahamishwa kuwa hadi sasa ni wazee 13,100 wasio kuwa na uwezo kati ya wazee 39,700 waliotambuliwa ambao wamepata vitambulisho hivyo vinawawezesha kupata matibabu bure”aliongeza Rubirya

Akizungumza kwa niamba ya wazee,mwenyekiti wa baraza hilo mkoa wa Njombe Papius Mvunyi amemshukuru mkuu wa mkoa wa Njombe kwa kutoa agizo hilo huku akisisitiza vitambulisho hivyo kuendana na utoaji wa huduma za afya bora kwa wazee.

“Nimshukuru mkuu wa mkoa kwa maagizo aliyoyatoa  hasa kwa wazee kupata vitambulisho vile ingawa kiuhalisia wengi wanalalamika vile vitambulisho havizingatiwi,nitawomba wazee kuelewa wanaokiuka na kuwafikisha mahali husika kwa kuwa sasa serikali inatuona”alisema Mvunyi

Vile vile wameomba miongozo kwa serikali juu ya mabaraza ya wazee ili waweze kwenda kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa wazee waliopo katika jamii kutokana na changamoto kubwa wanazozipata aggali wamelitumikia taifa kikamilifu wakati wakiwa na nguvu.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya akizungumza na baraza la wazee la mkoa wa Njombe mara baada ya kuzindua baraza hilo lililoambatana na uchaguzi wa viongozi.
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa baraza la wazee kutoka halmashauri zote za mkoa wa Njombe  waliofika kwenye uzinduzi wa baraza hilo kimkoa.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala akifurahia jambo na mwenyekiti wa baraza la wazee mkoa wa Njombe Papius Mvunyi mara baada ya uzinduzio wa baraza hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...