Na Said Mwishehe,Michuzi TV

JEZI mpya Klabu ya Simba kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2021/2022 zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Setemba 4 mwaka huu katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Kaimu Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema Simba iliingia mkataba mkubwa na Fred Vunja Bei kwa ajili ya jezi za Simba na waliingia mkataba wa Sh.bilioni mbili.

"Kabla ya Klabu ya Simba kuingia mkataba na Vunja Bei tulikuwa na Umbro na tulikuwa na mafanikio makubwa na Simba ni sehemu ya mafanikio.Tunafahamu biashara ya jezi na vifaa vya michezo ndio biashara kubwa duniani ,zaidi ya trilioni 84 zinapatikana katika biashara ya vifaa vya michezo na jezi,"amesema Kamwaga.

Ameongeza kuwa Simba katika kuamini vijana wa Tanzania imeamua kuingia mkataba na Fred Vunja Bei kwa ajili ya jezi na vifaa vya michezo vya Simba, ana maduka kila mahali na yote yatakuwa na jezi za Simba.

Aisha Kamwaga ameweka wazi kuwa Septemba utakuwa mwezi wa Simba kutokana na matukio mbalimbali yatakayoendelea kuanzia leo kuelekea Septemba 19 mwaka huu ambayo itakuwa Simba Day.

Kwa upande wake Fred Vunja Bei amesema kwamba wamepata nafasi ya kuaminiwa na Klabu ya Simba kutengeneza na kuuzaa jezi,hivyo nao wataonesha uaminifu na kuaminila kwao kwa vitendo.

" Simba imetuamini na sisi tutaonesha uaminifu, hakuna jezi ambayo imetengezwa ikavuja hadi sasa.Kwenye mitandao zimewekwa jezi nyinyi lakini ukweli jezi yetu haijavuja mpaka sasa.Jezi zetu za msimu huu zitazinduliwa Septemba 4 mwaka huu.

"Tutakuwa na wadau wa michezo kutoka sehemu mbalinbali, tumejipanga,tunajua ukubwa wa Simba,  hivyo uzinduzi wetu tutaufanya kwa ukubwa wa Simba,kutakuwa na uzinduzi wa aina mbili, Septemba 4 watazindua kuanzia saa 11 hadi saa tatu usiku,na itakuwa live Azam TV, na uzinduzi wa aina ya pili utakuwa wa mtandaoni kwa ajili ya kuuza jezi mtandaoni,"amesema Fred Vunja Bei.

Aidha amesema kuwa upatikanaji wa jezi , za Simba baada ya kuzinduliwa utakuwa tofauti na wengine, pale watakapokuwa wametambulisha tu jezi yao, basi kokote mwana Simba aliko ataweza kununua jezi muda huo huo wa kuanzia saa moja ya Septemba 4 mwaka huuu kokote aliko.

"Maduka ya Vunja Bei yatakuwa wazi saa 24 na mzigo utakuwa mwingi,hakuna atayakayekosa jezi ya simba na anataka kuuona ukubwa wa Simba kwa kununua jezi,"amesisitiza Vunja Bei.

Ameongeza kwa wale ambao watakwenda Simba Day watakuwa na punguzo la bei ya jezi ,hivyo tiketi za Simba zitauzwa na katika maduka ya Vunja bei.

Kaimu Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekie Kamwaga akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa jezi za Simba ambazo zitazinduliwa Septemba 4 mwaka huu

Mfanyabiashara maarufu wa mavazi  Fred Vunja Bei akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jezi za Simba ambazo watazindua Septemba 4 mwaka huu kuanzia saa saa moja jioni hadi saa tatu usiku jijini Dar es Salaam

Mwijaku akizungumza kuhusu jezi za Simba ambazo amesema zitakuwa nzuri kuliko jezi zote ambazo zimeshazinduliwa na vilabu vingine vya soka nchini ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Vunja Bei kwa kubeba jukumu la kusimamia jezi za Simba ambazo zitazinduliwa Septemba 4 mwaka huu.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...