Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imewataka Viongozi wa Dini zote nchini kuepuka migogoro baina yao wenyewe kwa wenyewe huku pia wakiwatakiwa kuepuka kuwa sehemu ya watu wanaochochea uvunjifu wa amani na taharuki katika jamii.
Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene katika ibada ya kuwekwa wakfu kuwa Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la Pentekoste PRA, Emmanuel Mogope jijini Dodoma.
Waziri Simbachawene amesema inashangaza kuona Kiongozi wa Dini anatumia nyumba ya Ibada kama sehemu ya kusuta wengine au kama kijiwe cha kuwapasha watu wasiowapenda jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya Mungu.
" Wakati mwingine tukiangalia madhabahu mengine ya Maaskofu katika baadhi ya Makanisa tunabaki kujiuliza inakuaje Askofu anatumia nyumba ya Ibada kama kijiwe cha kusuta wengine au kuwapasha wale wasiowapenda, hii inatufanya hata sisi tunaowafuata tuone kama tumepotea, ni vema kutumia nyumba za Ibada kuhubiri upendo, amani na mshikamano.
Lakini pia kumekua na kesi nyingi kwenye Ofisi yangu ambayo inashughulikia hizi Taasisi za Dini, kesi za migogoro ya Makanisa baina ya Askofu huyu na Askofu huyu hii pia naombeni sana viongozi wa Dini muhakikishe mnazimaliza tofauti zenu," Amesema Simbachawene.
Amesema migogoro mingi ambayo imekua ikiletwa ofisini kwake sababu kubwa huwa ni vyeo au fedha na hivyo kutoa wito kwa wachungaji waliowekwa kuwa Maaskofu leo kusimamia kanuni za taratibu zao ili kuepuka migogoro hiyo.
" Migogoro imekua ni mingi sana na hii inasababishwa na vyeo na fedha, Iko migogoro inasikitisha imefika hatua nasuluhisha migogoro mpaka nalia.
Wako Maaskofu wawili siwezi kuwataja majina kila siku wanalumbana hadi imefikia hatua napiga magoti kuwaomba wamalize tofauti zao, lakini cha kushangaza wanashindwa, niwaombe sana tushikamane yale mnayohubiri makanisani mwenu muyaishi pia na nyinyi," Amesema Simbachawene.
Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Taasisi za Dini zote kwani inaamini kupitia viongozi wa Dini ndio sababu pia ya amani na mshikamano uliopo katika Nchi yetu.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Wilson Aswile amshukuru Waziri Simbachawene kwa kutenga muda wake kushiriki katika ibada hiyo ya kuwaweka wakfu Maaskofu hao huku akiahidi kuendelea kulinda amani na mshikamano wa Kanisa hilo.
Askofu Mkuu Aswile pia ametoa ushauri kwa waumini wa Kanisa hilo nchini na watanzania kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa wa Corona ikiwa ni pamoja na kuridhia kwenda kuchoma chanjo kama ambavyo Serikali imekua ikishauri wananchi kufanya hivyo.
" Niipongeze Serikali chini ya Rais Samia tumeona utendaji wa kazi mzuri na unaoridhisha, tumpongeze pia Rais Samia kwa kusikia kilio cha watanzania na kupunguza tozo za miamala, lakini nitoe wito kwa watanzania kwamba suala la kulipa kodi ni muhimu na lina faida kwa Nchi yetu.
Niwashauri pia kuendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa wa Corona, msimsikilize yule mtu wenu, twendeni tukachanje, huu ugonjwa upo na Serikali imesema Chanjo ni hiyari lakini niwashauri muende mkachanje," Amesema Askofu Aswile.
Mbali na kuwekwa wakfu Askofu Mkuu Msaidizi, Emmanuel Mogope wengine waliowekwa wakfu ni Askofu Charles Malima ambaye anakua Askofu wa Kanda ya Kati na Askofu Daud Mkondya ambaye anakua Askofu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste PRA, Wilson Aswile akimuekea mikono, Askofu Emmanuel Mogope (aliyepiga magoti kulia) akimsimika kuwa Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa hilo leo jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika ibada ya kuwekwa wakfu kuwa Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la Pentekoste PRA, Askofu Emmanuel Mogope leo jijini Dodoma.

Waumini wa Kanisa la Pentekoste PRA jijini Dodoma wakifuatilia Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa hilo, Emmanuel Mogope pamoja na Maaskofu wengine wawili wa Kanda.

Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la Pentekoste PRA, Emmanuel Mogope (katikati), Askofu Charles Malima na Askofu Daud Mkondya wakila kiapo cha uaminifu cha kuwa Maaskofu wa Kanisa hilo leo jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akimpongeza Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la Pentekoste PRA, Emmanuel Mogope baada ya kusimikwa kushika nafasi hiyo leo jijini Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...