Na Amiri Kilagalila,Njombe

Tani 16,000 za mahindi wilayani Ludewa mkoani Njombe zinadaiwa kukosa soko endapo zoezi la ununuzi wa mahindi linalofanywa na wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula NFRA litafungwa kutokana na wakala huyo kununua tani 1000 pekee wilayani humo.

Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe wakili Joseph Kamonga  mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi wa mahindi kilichopo kijiji cha Mlangali na kupokea changamoto mbali mbali kutoka kwa wakulima waliofika na kuuza mazao yao.

“Ukiacha chakula,tuna tani za ziada 17,000 za mahindi lakini NFRA wamenunua tani 1000 pekee kwa hiyo tani 16,000 zinakosa soko”alisema Kamonga

Kamonga amesema nia kubwa ya kutembelea katika kituo hicho ni kutokana na malalamiko mengi aliyokuwa akiyapokea kutoka kwa wananchi wakati akiwa jijini Dodoma.

“Nia yangu ya kuja hapa ni kutokana na malalamiko mengi ambayo nikiwa bungeni Dodoma nilikuwa nikiyapokea kila siku bungeni mpaka hapakaliki.Kwenye bei pia mahindi yananunuliwa shilingi 430 kwa kilo,mwanzoni wananchi walishangilia waliposkia yanauzwa 500 kwa kilo lakini baadaye yakaanza mabadiliko ya bei hii imeleta malalamiko sana kwa wakulima na wanahofu hapa katikati amebadilisha kumbe toka mwanzo wangekuwa wametoa bei elekezi kwa kila eneo hii ingepunguza malalamiko”

Katika hatua nyingine amesema wananchi wakulima wamekuwa na changamoto ya kusafiri umbali mrefu na wengine wakisafiri KM 78 kufuata kituo cha ununuzi wa Mahindi kilichopo kijiji cha mlangali huku awali katika wilaya hiyo kulikuwa na vituo vitatu.

“Kwa miaka mingi Ludewa kumekuwa na vituo vitatu,kumekuwa na kituo cha Ludewa vijijini,Mlangali pamoja na kituo cha Shaurimoyo nah ii imekuwa ikiwarahisishia wakulima kufikisha mazao kwenye soko kirahisi lakini kwa sasa tumewaongezea mzigo mkubwa sana wakulima”aliongeza Kamonga

Kutokana na changamoto hizo mbunge huyo wa Ludewa amesema wananchi wana imani kubwa na ununuzi wa mahindi unaofanywa na wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) huku akiahidi kushughulikia changamoto zilizojitokeza ili kuwasaidia wakulima wa jimbo la Ludewa.

Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe wakili Joseph Kamonga akiwa amebeba gunia la mahindi na kulifikisha ndani katika kituo cha kununua mahindi kilichopo kata ya Mlangali wilayani Ludewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...